Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizindua rasmi
albam mpya ya mwimbaji Goodluck wakati wa tamasha la Pasaka
lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza , Wabunge pamoja na
Maaskofu wa makanisa ya Mwanza.
Tamasha
hilo ambalo limehudhuriwa na mashabiki wengi mkoani humo limetumbuizwa
na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili kutoka hapa nchini na nchi
jirani za Zambia na Kenya, waimbaji hao ni Upendo Nkone , Martha baraka ,
Jesca BM, Joshua Mlelwa , Tumsifu Rufutu, Christopher Mwahangila,
Jeniffer Mgendi, Bonny Mwaiteje, Goodluck ambaye amezindua albam yake
mpya na waimbaji Faustine Munishi kutoka nchini Kenya, Solomon Mukubwa
kutoka Nchini Kenya pamoja na Ephraim Sekereti kutoka nchini Zambia wote
kwa pamoja wamefanya maonesha mazuri yaliyopagawisha mashabiki wa
muziki wa injili katika uwanja wa CCM Kirumba na kuwafanya wacheze kila
wakati, katika picha kulia ni mwimbaji Goodluck na kushoto ni Bw. Alex
Msama Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha
hayo.
Tamasha
hilo litaendelea kesho kwa onesho kabambe linalotarajiwa kufanyika
mjini Kahama mkoani Shinyanga baada ya kumaliza maonyesho mawili katika
mikoa ya Geita na Mwanza.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MWANZA)
Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wa nne kutoka
kulia akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela alipokuwa
akimkaribisha rasmi ili kutoa salam zake kutoka kwa serikali.
Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akishiriki katika
sala maalum ya kuombea albam ya mwimbaji Goodluck wa pili kutoka kulia
iliyotolewa na maaskofu wa mwanza kabla ya kuizindua
Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akishuka kutoka
jukwaani kwa ajili ya kuizindua rasmi albam hiyo na kutoa salaam za
serikali katika tamasha la Pasaka.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela akipokewa na Mkuu wa wilaya ya
Nyamagana Mh. Baraka Konisaga kushoto na Mkurugenzi wa Msama Promotion
Bw. Alex Msama wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza.
Mkuu
wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga akipokewa na Mkurugenzi wa
Msama Promotion Bw. Alex Msama wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu akiinunua albam ya mwimbaji Goodluck mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye kwenye tamasha la
Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akitoa salam zake
na kukemea watu wanaojihusisha na wizi wa kazi za wasanii na kusema
serikali ya awamu ya tano itahakikisha wahusika wote wanashughulikiwa
vya kutosha ili kuhakikisha wasanii wanapata haki yao katika kazi zao na
jasho lao.
Mwimbaji
Goodluck akiimba mara baada ya kuizindua rasmi albam yake kwenye
tamasha la pasaka jijini Mwanza lililofanyika kwenye uwanja wa CCM
Kirumba.
Mwimbaji Upendo Nkone akifanya vitu vyake jukwaani na kuwarusha vya kutosha mashabiki waliohudhuria katika tamasha hilo.
Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiongoza na
viongozi mbalimbali pamoja na baadhi ya maaskofu kucheza wakati mwimbaji
Upendo Nkone alipokuwa akiimba jukwaani.
Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipiga picha ya
pamoja na waimbaji wa muziki wa injili mara baada ya tamasha hilo
kumalizika kutoka kulia ni Bonny Mwaiteje. Jesca BM na Upendo Nkone.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akicheza wakati mwimbaji Bonny Mwaiteje alipokuwa akitumbuiza.
Mwimbaji Bonny Mwaiteje akifanya vitu vyake jukwaani
Mkuu
wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga akipunga mkono huku akicheza
na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Mwanza na maaskofu pamoja na
wachungaji wakati mwimbaji Upendo Nkone akifanya vitu vyake jukwaani.
Roho
wa Bwana Yesu akiwashukia mashabiki wa muziki wa injili wakiwa
wamenyanyua mikono yao juu juu wakati mwimbaji Upendo Nkone alipokuwa
akiimba jukwaani.
Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion pamoja na Mkewe wakielekeakuketi jukwaa kuu.
Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipokelewa na
Alex Msama na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela alipowasili uwanja
wa CCM Kirumba.
Mwimbaji Martha Baraka akitumbuiza katika tamasha hilo.
Naye Mwimbaji Jeniffer Mgendi akafanya mambo makubwa jukwaani kama anavyoonekana.
Bw. Alex Msama kulia akiwa na Mkewe katikati pamoja na MC wa matamasha ya Pasaka MC Mwakipesile.
Mmoja wa washabiki ambaye ni mlemavu alishindwa kujizuia akaamua kucheza kama anavyoonekana katika picha.
Mwimbaji Joshua Mlelwa amefanya mambo makubwa jukwaani katika tamasha hilo kama kawaida yake.
Mashabiki wakicheza kwa furaha katika tamasha hilo.
Mwimbaji Faustine Munishi kutoka nchini Kenya akipagawisha mashabiki na nyimbo zake za kuabudu kama vile "Malebo".
Mwimbaji Christopher Mwahangila akiwapa upako mashabiki kupitia injili ya uimbaji.
Mwimbaji Ephraimu Sekereti kutoka nchini Zambia naye akaimba nyimbo za kusifu na kuabudu.
Solomon Mukubwa akiafunga kazi na nyi,bo zake kali zilizowafanya mashabiki kuwa wima wakati wote kama wanavyoonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni