KARATASI ZA KUPIGIA KURA ZAWASILI ZANZIBAR

Karatasi za kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa marejeo wa Machi 20, 2016 zimewasili Zanzibar zikitokea nchini Afrika ya kusini.


Kura hizo utengezaji wake umegharimu Sh. bilioni 4.5 kwa ajili ya idadi ya wapiga kura.

Karatasi hizo zimewasili majira ya saa nane mchana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar baada ya kuteremshwa zimepelekwa katika ghalani kuhifadhiwa zikisubiri tarehe ya kusambazwa.

Viongozi mbali mbali wameshuhudia akiwemo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha na baadhi ya Makamishna wa Tume hiyo, pamoja na viongozi wa vyama vya Siasa Zanzibar kikiwemo Chama cha TADEA, CCM na baadhi ya waangalizi wa ndani wa vyama .

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Ndg. Salum Kassim Ali, amesema pia wamepokea vifaa vya nukta nundu elfu 2000 kwa ajili ya watu wasioona, na wanatarajia kuanzia Machi 17 zitasafirishwa kisiwani Pemba na siku inayofuata ya Machi 18 zitaanza kugawia katika Wilaya za Unguja.

                                                                                         Kwa hisani ya ZanziNews

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni