Wafanyakazi
wa kiwanda cha TBL cha Arusha wakifanya mazoezi ya kukimbia wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya Afya Kwanza mwishoni mwa wiki
Meneja
wa kiwanda cha TBL mkoa wa Arusha,Salvatory Rweyemamu akipiga mpira
kuashiria kuanzishwa kwa kampeni ya Afya Kwanza iliyoanzishwa na TBL
Group kwa lengo la kuimarisha afya za wafanyakazi wake.
Meneja Uendeshaji wa taasisi ya AAR Insurance Tanzania Ltd, Dk Harold
Adamson akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha TBL mkoa wa Arusha juu
ya umuhimu wa kuimarisha afya zao kwa kufanya mazoezi wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya Afya Kwanza uliofanyika kiwandani hapo mwishoni
mwa wiki.Wafanyakazi
wa TBL kiwanda cha Arusha wakimsikiliza mtaalamu wa lishe huku
wakijipatia matunda baada ya kufanya mazoezi ya kuimarisha viungo vyao
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Afya Kwanza iliyofanyika kwenye
kiwanda hicho eneo la Themi jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
………………………………………………
Kampeni ya TBL Group imezindua
kampeni ya kuimarisha afya za wafanyakazi wake wote ambapo wanashiriki
kufanya mazoezi ya mwili sambamba na kupatiwa kupatiwa elimu
inayohusiana na lishe bora na matumizi ya vyakula visivyo na athari.
Afya Kwanza ambayo imeanzia kwa
wafanyakazi waliopo Makao makuu na viwanda vilivyopo jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki imezinduliwa katika kiwanda cha Arusha na
kushirikisha wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Msimamizi wa Programu hii ,Julieth
Mgani alisema kuwa itakuwa endelevu na wafanyakazi wameonekana
kuifurahia katika kipindi cha muda mfupi tangia ianzishwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni