Mkuu  
mpya  wa  Mkoa  wa  Kagera,Meja  Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu 
amewaagiza  watumishi  wasio  na  sifa za  kuajiriwa kujiondoa  kabla  
ya March  31  mwaka  huu.Kijuu  alitoa 
 kauli  hiyo  jana  wakati  wa  Makabidhiano  ya  ofisi baina  yake  na 
 mkuu  wa  mkoa  wa  zamani,John Mongella ambapo alisema  kwamba  
Tanzania  inawatumishi  hewa  zaidi  ya 2000, hivyo ana imani  hata  
Kagera  wapo.
"Hao watumishi  hewa  endapo  watang'ang'ania kubaki katika vitengo  walivyopo  nitawashughulikia wahusika  wakuu  wa  vitengo  hivyo," alisema
Aidha,
 aliagiza wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kusimamia uundwaji wa 
mabaraza  ya  usuluhishi kuanzia ngazi za kata hadi  mkoa  ili  
kusimamia  haki  za  wananchi.
Pia  
aliwataka  watumishi  wa  serikali  mkoani  humo kufahamu maudhui ya 
"Hapa Kazi Tu", kwa kufanya kazi kwa kasi,haraka, nguvu, maarifa  na  
uadilifu.
Aliwataka 
 kutosubiri  kusukumwa, lakini wajitambue wao ni akina  nani na  
wanapaswa  kufanya  nini  kutokana  na  majukumu  waliyopewa.
Alisema  
ili  kufikia  lengo  la  Rais John Magufuli la kuwatumikia wananchi  
kwa  uaminifu  ni  lazima  kushikiria  uadilifu  na  kutambua  kwamba 
watumishi wapo kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni