Wasanii
wa Kituo cha Utamaduni kilichopo chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wilaya
ya Arumeru mkoani Arusha wakicheza ngoma ya Sindimba wakati Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
Wambura (hayupo pichani) alipotembelea kituo hicho hivi karibuni kwa
ajili ya kuona shughuli za kitamaduni zinazofanyika kituoni hapo.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(wa pili kulia) akiwaangalia wasanii wa Kituo cha Utamaduni kilichopo
chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wilaya ya Arumeru mkoani Arusha (hawapo
pichani) wakicheza ngoma ya kabila la wa Meru wakati alipotembelea
kituo hicho hivi karibuni kwa ajili ya kuona shughuli za kitamaduni
zinazofanyika kituoni hapo. Kulia ni Randall Stubbs ambaye ni Meneja
Mradi wa kituo hicho kinachojengwa chuoni hapo, watatu kulia ni Afisa
Michezo wa Mkoa Mwamvita Okeng’o na wa nne kulia ni Afisa utamaduni
wilaya ya Arumeru Senyael Pallangyo.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akiangalia mchoro wa ramani ya Kituo cha Utamaduni kinachojengwa katika
chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo wilaya ya Arumeru mkoani
Arusha wakati alipotembelea kituo hicho hivi karibuni kwa ajili ya kuona
shughuli za kitamaduni zinazofanyika kituoni hapo. Kulia ni Afisa
utamaduni wilaya ya Arumeru Senyael Pallangyo akifuatiwa na Randall
Stubbs ambaye ni Meneja Mradi wa kituo hicho.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Kituo cha
Utamaduni kilichopo chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo wilaya ya
Arumeru mkoani Arusha wakati alipotembelea kituo hicho hivi karibuni kwa
ajili ya kuona shughuli za kitamaduni zinazofanyika kituoni hapo.
Picha na wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni