Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba yake katika semina hiyo. Kushoto ni
Mwasisi wa Taasisi ya Millen Magese, Millen Happiness Magese. (Picha na Video na Andrew Chale,Modewjiblog).
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi
Kigwangalla (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mwanadada, Millen
Happiness Magese (katikati) pamoja na Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni,
Bw. Rogers Shemwelekwa.
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
imesema kuwa ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali akiwemo
Mwanadada Millen Magese na Taasisi yake katika mapambano ya ugonjwa na
athari za Endometriosis ambao unawapata wanawake wengi hapa nchini.
Kauli
hiyo imetolewa mapema leo Machi 30.2016 na Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla
wakati wa kufungua rasmi semina maalum kwa vijana wapatao 500 wa shule
za Sekondari zikiwemo za Turiani Sekondari,Makurumla na zinginezo za
Manispaa ya Kinondoni pamoja na walezi na walimu, ambapo katika mkutano
huo, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, juhudi zinazofanywa na Mwanadada
Millen Magese ni za kuungwa mkono hivyo wataendelea kushirikiana naye
bega kwa bega.
Dk.
Kigwangalla amebainisha kuwa, anatambua wanawake wengi duniani kote
wanasumbuliwa na tatizo hilo ambapo gharama zake kwa kawaida ni kubwa
huku bado wataalam wanaendelea kushughulikia namna ya upatikanaji wa
tiba yake ili kuweza kuwa nafuu.
“Napongeza
juhudi za dhati zinazofanywa na taasisi ya Millen Magese, katika kuunga
mkono juhudi za serikali ya tano kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto za kuwasogeza wananchi karibu na huduma
bora kwa ajili ya Maendeleo na Ustawi wa Jamii yetu.
Tatizo
la kutoshika mimba (kitaalamu Endomytiosis) hutokana na sababu
mbalimbali, nyingi zikichangiwa na uelewa mdogo wa jamii inayomzunguka
msichana au mama anayejianadaa kuanza kubeba mimba, lakini pia upungufu
wa vifaa tiba hospitalini na kwenye vituo vya afya sambamba na
kukosekana kwa wataalamu katika hospitali zetu, Hivyo tunapenda kuchukua
fursa hii kupongeza juhudi kama hizi za kuandaa semina na warsha ikiwa
ni hatua madhubuti na ya msingi katika kuikabiliana na changamoto ya
uelewa wa tatizo hili katika jamii.
Kwani,
tunaamini, limekuwa jambo la faraja sana, tangu Magesse alipojitokeza
hadharani na kuihabarisha dunia juu ya tatizo hili linalomkabili yeye
binafsi. Naomba kusema wazi kuwa, huo ulikuwa uthubutu wa pekee wa
mrembo huyo, kiasi cha kuifanya jamii kubwa ya kimataifa kuanza
kulifuatilia tatizo hili ili kusaidia mabinti wadogo ambao walikuwa
hawajakumbwa na hali hiyo. “ alieleza Naibu Waziri Dk. Kigwangalla
katika hotuba yake hiyo.
Aidha,
Dk. Kigwangalla aliongeza kuwa, ni faraja kubwa kwa watanzania tangu
Magese Foundation ilipoanzishwa ikifanya kazi kubwa ya kuhamasisha
upatikanaji wa vifaa na pia ujenzi wa hospitali maalumu kwa ajili ya
kutibu tatizo hilo. Jambo hilo linaendelea kuitia moyo serikali hususani
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kufikia
lengo la kumuwezesha mtoto wa kike kufikia malengo tarajiwa.
Kwa
upande wake, Mwanadada Millen Magese amewaeleza vijana wa kike katika
semina hiyo kuwa, wawe wazi pindi wajisikiapo dalili mbalimbali wakati
wanapokuwa katika mzunguko wa siku zao ambapo na kubainisha kuwa, jambo
hilo endapo litabainika mapema ni rahisi kulipatia tiba kuliko kuficha
na kufika steji mbaya.
Mwanadada,
Millen Magese pia alitumia wasaha huo kuishukuru Serikali kwa namna
walivyokubaliana kushirikiana naye bega kwa bega katika mapambano dhidi
ya tatizo hilo hapa nchini ambapo pia amewashukuru wadau wote kwa kuwa
naye dhidi ya mapambano hayo.
Semina
hiyo pia imeweza kukusanya watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu
wasanii, wanamitindo na wabunigu wa mavazi, wafanyabiashara na
wanaharakati wanawake katika maendeleo hapa nchini huku wanaume nao
wakijumuika pamoja ilikusambaza ujumbe huo kwa wenza wao na marafiki
zao.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
Mwanadada, Millen Happiness Magese.
Baadhi ya wanafunzi, wadau wanaosaidiana na mwanadada Millen Magese wakifuatilia semina hiyo.
Baadhi
ya wageni waalikwa, wakiwemo waliowahi kushiriki mashindano ya
ulimwende hapa nchini ..wakiwa wamejumuika pamoja kuungana na taasisi ya
Millen Magese.
Wanafunzi wakifuatilia semina hiyo.
Wanafunzi wakifuatilia semina hiyo.
Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Bw. Rogers Shemwelekwa akitoa hotuba fupi katika semina hiyo
Baadhi
ya wadau walioungana kwa pamoja kusaidiana na taasisi ya Millen Magese
wakifuatilia semina hiyo. Mustafa Hassanali pamoja na Rio Paul ambao
wote ni wabunifu wa mavazi hapa nchini.
Seven Mosha na Miss Tanzania 2008, Nasreen Kareem.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, akitoa hotuba yake.
Mmoja wa madaktari bingwa wa wanawake wa Hospitali ya Muhimbili akitoa maelezo machache.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni