DONALD TRUMP AHAIRISHA MKUTANO WAKE CHIGACO KUFUATIA GHASIA

Muwania urais wa Marekani Donald Trump amehairisha mkutano wake wa hadhara Jijini Chicago baada ya maandamano ya kumpinga mgombea huyo wa Republican kugeuka kuwa ghasia.

Mamia ya waandamanaji walikusanyika kwenye ukumbi wa mkutano huo katika Chuo Kikuu cha Illinois saa kadha kabla ya Trump kufika.

Ndani ya ukumbi huo mapigano yaliibuka baina ya wafuasi wa Bw. Trump na watu wanaompimga waliokuwa na bendera huku wakipaza sauti za kumshutumu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni