MKURUGENZI TBC ANUSURIKA KATIKA AJALI KASULU


 Gari la Mkurugenzi wa TBC, Dk Ayoub Rioba likiwa limepinduka baada ya lupata ajali.
Na Rhoda Ezekiel, FK Blog Kigoma.
WATU wawili wamepoteza maisha huku Mkurugenzi wa Shirika la utangazaji TBC Ayub Rioba amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Kibondo kwenda Kigoma mjini kupata ajali katika  Kijiji cha Mgombe Kata ya Nyakitonto Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Akizungumza leo mara baada ya tukio hilo Kamanda wa Polisi Kigoma, Martini Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majinia ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto na Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto ambae hali yake ni mbaya na anendelea naatibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

Alisema katika ajali hiyo Waliokuwemo kwenye gari mbali na Dk Rioba ni Mkurugenzi wa Vipindi TBC na Meneja wa Vipindi Kanda ya Magharibi Zabron Mafuru na Dereva aliefahamika kwa jina la Abubakari ambapo wao wamepata majeraha madogo madogo na wamepatiwa matibabu na wanaemdelea vizuri.

Kamanda Otieno alisema Chanzo cha ajari hiyo ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo na kuwaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.

MPANGO WA PAMOJA WA TANZANIA NA CHINA KATIKA KUONGEZA UZALISHAJI WA TIJA WA ZAO LA MAHINDI MKOANI MOROGORO WAZINDULIWA


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin, akimuonyesha Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, moja ya picha katika Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini, katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji hicho. Mradi huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro na Chuo hicho Kikuu cha Kilimo cha China. Nyuma yao ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro.
 Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo, akisalimiana na Profesa Wu Jiu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China alipowasili kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji  cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro.  
 Wasanii akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi,  jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro.
 Balozi wa Tanzania hapa nchini Wang Ke akisaini kitabu ca wageni alipowasili kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba moani Morogoro. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa mkoa huo Regina Chonjo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro
 Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe (mwenye gauni la bluu) na Regina Chonjo wakiselebuka muziki na wananchi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji hicho mkoani Morogoro. 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani humo.
 Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro. 
 Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani humo.
 Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba Mikese mkoani Morogoro.
 Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji hicho cha Mtego wa Simba.
 Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, akipongezwa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo baada ya hotuba yake. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya gairo Siriel Mchembe  
 Benjamin Amos akizungumza wati wa uzinduzi wa kwanza wa Jumuiya ya Waliosoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha China. uzinduzi huo ulienda pamoja na uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba Mikese mkoani Morogoro.
 Waliosoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha China waakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya uzinduzi wa Jumuiya ya Waliosoma katika Chuo hicho
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin (kushoto ) na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo na Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke (kulia) wakijiandaa kufungua mabango yenye maelezo, wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin (kushoto ) na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo wakifungua bango lenye maelezo wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
 Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, wakifungua bango lenye maelezo wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
 Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke wakifurahi baada ya kufanya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin (kushoto ) na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo wakionyeshana bango lenye maelezo baada ya kuzindua jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
Balozi wa China hapa nchini Wang Ke (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Cha China na Viongozi wa mkoani Morogoro baada ya uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

HOSPITALI DAR ZABAINIKA KUWA NA WAGONJWA WENGI WALIOKUFA KWA VIFO VYA MALARIA, UKIMWI


Mganga Mkuu wa Serikali, Prof Muhammad Bakari Kambi akizungumza wakati akifungua mdaharo uliowahusisha wataalamu mbali mbali kujadili ni kitu gani kinasababisha vifo katika hospitali, kufuatia utafiti uliofanywa na  Taasisi ya Taifa Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMRI). Kupitia matokeo ili kutoa ushauri wa kisera ili serikali iweze kutilia mkazo ambapo Prof. Kambi amesema changamoto inazikumba hospitali nyingi ni magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa ni changamoto kubwa inayopelekea kuzigharimu sana. Kaimu Mkurugenzi wa NIMRI akimkaribisha mgeni rasmi. 
 Washiriki kutoka taasisi mbali mbali za serikali na hospitali za mikoa wakifuatilia kwa makini.
 Mgeni rasmi akiwa na Washiriki kutoka taasisi mbali mbali za serikali na hospitali za mikoa.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

 HOSPITALI za Mkoa wa Dar es Salaam zimebainika zilikuwa na wagonjwa wengi ambao walikufa kutokana na malaria, Ukimwi , ajali, maambukizi ya bakteria kwenye damu, upungufu wa damu, saratani na kifua kikuu(TB) ukifuatiwa na mkoa wa Morogoro. Imefahamika malaria na upungufu wa damu ulichangia vifo vingi kwenye kundi la watoto chini ya miaka mitano na vifo kutokana na Ukimwi na Kifua Kikuu viliathiri zaidi kundi la watu wazima, vifo vinavyotokana na ajali viliathiri zaidi kundi kubwa la vijana wakati saratani ziliathiri makundi ya umri wote. 

 Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) wakati ikielezea matokeo ya utafiti wa vifoo vinavyotokea katika hospitali za Tanzania. Imeelezwa na NIMR taarifa za vifo ni moja ya vyanzo muhimu vya takwimu katika kupanga mipango na kuandaa sera ya afya ambapo uchambuzi wa takwimu katika makundi ya magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukiza na kundi la ajali na majeraha ulionesha tofati kubwa kati ya mikoa na mikoa. 

 Utafiti huo umebaini mikoa ya Pwani, Geita na Katavi imeonekana kuathirika zaidi na magonjwa ya kuambukiza na utapia mlo. Wakati vifo kutokana na ajali na majeraha viliathiri zaidi mikoa ya Rukwa, Tabora, Singida na Kigoma. Kundi la magonjwa yasiyoambukiza limeathiri zaidi mikoa ya Ruvuma, Manyara, Dar es Salaam na Mwanza.

 "Kati ya mwaka 2006 na mwaka 2015, mikoa ya Kanda ya Kati (Dodoma, Singida, Manyara) mikoa ya kaskazini (Arusha na Kilimanjaro) ndiyo iliyobeba mzigo mkubwa wa vifo vilivyosababishwa na maradhi ya mifumo ya kupumua, upungufu wa damu uliathiri zaidi mikoa ya Dodoma, Simiyu na Mtwara,"imesema. Imeeleza utafiti umeanisha changamoto katika ukusanyaji, uchanganuzi na matumizi ya takwimu katika hospitali zilizopo nchini na kumekuwa na matumizi hafifu ya majina rasmi ya magonjwa kwa kutumia mwongozo wa kimataifa. 

 "Vyanzo vikuu vya vifo hospitalini nchini Tanzania ni pamoja na malaria, maradhi yanayoathiri mfumo wa kupumua, Ukimwi, upungufu wa damu na magonjwa ya moyo. "Kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya watoto wachanga na magonjwa ya mfumo wa kupumua katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. 

 Mapendekezo ya utafiti huo Serikali kuandaa mwongozo thabiti wa ukusanyaji, matumizi, utunzaji na uhifadhi bora ya takwimu za afya,"amesema NIMR. Pia pendekezo lingine ni kujenga uwezo wa watumishi wa afya katika uchanganuzi na matumizi ya takwimu, kuimarisha mfumo wa takwimu wa kielektroniki na kuimarisha mafunzo ya madaktari katika utumiaji wa mwongozo wa kimataifa wa kuainisha vyazo rasmi vya maradhi na vya vifo. Imefafanua zaidi kuhusu utafiti huo amesema kuanisha vyanzo vya vifo katika hospitali zetu ni muhimu kufuatilia matukio ya vifo, kutathimini ubora wa huduma zinazotolewa na kuanisha vipaumbele katika huduma za afya.

 "Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuanisha matukio ya vifo katika hospitali za Tanzania ili kutambua maradhi yanayoathiri jamii yetu. Utafiti pia ulichunguza uwepo,upatikanaji, utunzaji na ubora wa takwimu za vifo hospitalini,"imeongeza. Kuhusu mbinu za utafiti huo, inaeleza ulifanyika kuanzia Julai hadi Desemba mwaka 2016 na ulihusisha hospitali 39. Hospitali hizo ni pamoja na hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa, Hospital Maalum na hospitali za Wilaya.

 "Taarifa za vifo vilivyotokea kuanzia mwaka 2006 had mwaka 2015 zilikusanywa.Takwimu hizo zilipatikana kutoka kwenye rejesta za hospitali na vibali vya mazishi kutoka kwa Wakala wa Vizazi na Vifo katika ofisi za Wilaya. "Taarifa zilizokusanywa zilihusu jinsia ya mgonjwa, tarehe ya kulazwa hospitali, tarehe ya kufariki na sababu za kifo. Vyanzo vya vifo viliwekwa katika makundi 45 kulingana na utaratibu wa makundi ya magonjwa wa Shirika la Afya Duniani,"imesema. 

 Kuhusu matokeo, amesema jumla ya hospitali 39 zilishiriki katika utafiti huu. Kwa ujumla kulikuwa na ugumu katika upatikanaji wa takwimu na utunzaji wa takwimu katika hospitali nyingi ulikuwa una mapungufu makubwa. "Baadhi ya takwimu hazikupatikana katika baadhi ya hospitali au katika baadhi ya miaka.Utunzaji wa takwimu ulikuwa mzuri kiasi katika hospitali za rufaa za kanda kuliko za mikoa na wilaya.

 "Matumizi ya majina ya magonjwa kwa kufuata mwongozo wa kimataifa yalikuwa hafifu. Baadhi ya dalili za ugonjwa ziliandikwa kama ndiyo sababu za kifo. Jumla ya vifo 247,976 vilitolewa taarifa katika kipindi cha miaka 10 (2006-2015). Kulikuwa na tofauti kubwa katika idadi ya vifo kati ya jinsia ya kiume na ya kike,"imesema NIMR wakati inaelezea utafiti huo.

KIKAO CHA RAIS MAGUFULI,WAFANYABISHARA KIWE CHACHU YA MAENDELEO KATIKA NCHINI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KWA Ujinga wangu naomba niseme mapema tu, mimi si mfanyabiashara ila 
nimekuwa karibu kwasababu nanunua bidhaa za wafanyabishara.

Nanunua bidhaa za wafanyabishara kulingana na mahitaji yangu ya kila 
siku.Ndio ukweli maana maisha yangu ni kwamba nikijipata vijesenti naenda dukani nanunua nachojitaji.Kwa kuwa nimekuwa karibu na wafanyabishara , nikiri nimekiwa nikifuatilia 

mambo yao mbalimbali.Hata wanapotoa malalamiko yao kuhusu kukwamishwa kwa mambo yao nimekuwa nikisia.Malalamiko ya tozo kubwa za kodi kwenye masuala ya biashara nayo nimekuwa nikiwasikia wafanyabishara wakilalamika.

Nawasikia kwasababu mbali ya kuwa ni sehemu ya mteja wao , bado nami ni Mtanzania ambaye nashukuru Mungu ni muumini wa kufuatilia kila jambo nchini kwetu.Hata Rais wangu Dk.John Magufuli wakati unatoa maagizo kwa Waziri wa Fedha na Mpango kukaa na Mamalaka ya Mapato Tanzania(TRA)kuangalia namna ya tozo za kodi.

Ukasema kuwa kodi zimekuwa kubwa kiasi cha kufanya kuwa kero.Ukaeleza 
namna ambavyo unataka kodi iwe jambo la heshima kwa Taifa na si kuwa kero kwa mlipaji.Kwa Ujinga Wangu baada ya kusikia utakutana na wafanyabishara kutoka maeneo mbalimbali nchini.Nikasema kwenye mazungumzo hayo lazima kitaeleweka.

Rais Magufuli ukaamua kutoa nafasi ya kila mfanyabishara kutoa dukuduku lake.Nakumbuka kwenye mkutano huo ambao wewe uliongoza ulieleza namna ambavyo unataka kumsikia kila mmoja wao.Wafanyabishara nao kwa kuwa kuna mambo ambayo yalishikuwa kero kwao waliamua kusema kila kitu.Hakuna ambacho wamekificha maana waliona ndio sehemu pekee ya wao kusikilizwa.

Wakaeleza changamoto ambazo wanakutana nazo kutoka kwa TRA.Wakaeleza namna ambavyo wanaojihusisha na biashara ya mazao kuharibikia njiani.Wakaeleza namna ambavyo wanatamani Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya biashara.Wafanyabishara hao wakaelezea mambo mengi.Wakaeleza namna ambavyo wanaamini kikao hicho kati yao na Rais kitakuwa na mafanikio makubwa.Kama nilivyotangulia kueleza awali mimi si mfanyabiashara lakini nimevutiwa na mazungumzo kati ya pande hizo mbili.

Kw Ujinga wangu nikawa nawaza kwanini kikao hichi kimechelewa kufanyika?Hata hivyo nikajijibu mwenyewe kuwa ratiba yako imebana kutokana na majukumu mbalimbali ya kuwatumikia Watanzania.Kwa mtazamo wangu kikao hicho kitakuwa chachu ya maendeleo ya nchi yetu.Tunatambua mchango wa wafanyabishara katika kujenga uchumi wa nchi yetu.

Natambua TRA kutokana na makadirio ya kodi kuwa juu , kuna wafanyabishara wengi wamefunga maduka yao.Wameyafunga si kwasababu wanapenda bali mazingira ya kodi yamekuwa kikwazo kwao.Nieleze ni kweli kuna malimbikizo ya madeni ya kodi ambayo wafanyabishara wanadaiwa lakini nilidhani TAR wangekuwa na jukumu la kukaa na wafanyabishara na kisha kuangalia njia nzuri ya kuhakikisha madeni yanalipwa na wafanyabishara wanaendelea kufanyabishara.

Naamini kikao kati ya Rais Magufuli na wafanyabishara kitafungua ukurasa mpya katika sekta ya biashara nchini.Rais wakati anazungumza kwenye kikao hicho alitumia nafasi hiyo kushughulikia baadhi ya malalamiko.Akatumia nafasi hiyo kutoa maagizo na maelekezo kulingana na hoja za wafanyabiashara.

Hata hivyo kukosekana kwa baadhi ya mawaziri au makatibu wakuu kwenye kikao hicho kilisababisha Rais Magufuli kuhoji kwanini hawakufika.Sababu ya kuwaliza ilitokana na kuamini kuna baadhi ya mambo yanaweza kushughulikiwa na wizara moja kwa moja.

Pamoja na kukosekana kwa baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu ambao nao walialikwa kwenye kikao hicho bado lengo la mkutano ulifanikiwa.Hakika mkutano huo umefungua ukurasa mpya kati ya Rais Magufuli na wafanyabishara.Sote tunafahamu kuna wakati ilijengeka dhana kuwa hakuna uhusiano mzuri kati ya wafanyabiashara na Serikali.Hata hivyo unapomsikiliza Rais Magufuli na wafanyabishara hao unabaini hakuna tatizo bali yapo mambo yaliyokuwa yanasababisha manung'uniko.

Kabla ya kuhitishwa kwa kikao hicho, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipata nafasi ya kutoa maelezo yake na akatumia nafasi hiyo kuonesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya maofisa wa TRA kuwa kero katika eneo la ukusanyaji kodi.Akasema wamesababisha kufungwa kwa maduka bila sababu za msingi na akatumia nafasi hiyo kuelezea hatua ambazo amechukua kukomesha tabia hiyo.

Wakati Rais Magufuli wakati anahitimiza kikao hicho, amesema yapo baadhi ya mambo ufumbuzi wake utakuwa wa haraka na mengine watakwenda kujipanga ili kutafuta ufumbuzi wake.

Akawaambia wafanyabishara hao kuwa katika utawala wake watatajirika sana na anachokifanya ni kuondoa kona kona ambazo zimekuwa zikikwamisha wengine.Akaleza namna ambavyo baadhi ya wafanyabishara wanatozwa kodi kubwa na wengine hawatozwi kodi.

Akawahakikishia kuwa Serikali yake inawapenda wafanyabiashara na itakuwa nao bega kwa bega.Rais akasema katika eneo la uchumi kuna vita kubwa na hivyo ni Watanzania kwa umoja wao kusimama imara.Ni maoni yangu kuwa Rais Magufuli baada ya kikao hicho kuna mengi ambayo ameyapata kutoka kwa wafanyabishara hao na yakifanyiwa kazi tutasonga mbele.

Kwa Ujinga Wangu naomba nieleze wazi kikao hicho kimenifanya hata mimi nisiye mfanyabishara nianze kufikia kufanya biashara kwani mazingira ya biashara chini ya Rais yanayonekana kuanza kuwa bora zaidi.Ahsante kwa kunisoma
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  alipokuwa akiendesha  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam hivi karibuni 

WCF YAWAELIMISHA MAAFISA WAAJIRI KUHUSU MISINGI YA KULINDA USALAMA NA AFYA ZA WAFANYAKAZI MAHALA PA KAZI


 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, (aliyesimama), akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina juu ya masuala ya msingi ya kulinda usalama na afya mahala pa kazi na Fidia kwa wafanyakazi kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, (JNICC), jijini Dar es Salaam Machi 22, 2018. Wengine pichani  I Mkurugenmzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (katikati), na Meneja wa Tathmini ya hatari mahala pa kazi, (Workplace Risk Assesment Manager), Bi. Nanjela Msangi.



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

NIWAJIBU wa mwajiri kutoa taarifa kwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ya kuumia kwa mfanyakazi wake ikiwa ni pamoja na kifo.

Hayo yamesemwa leo Machi 22, 2018, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, wakati akifungua semina ya siku moja iliyowaleta pamoja mameneja na maafisa waajiri kutoka sekta ya umma na binafsi jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Wafanyakazi, (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Pia ni wajibu wa mwajiri kumpatia vifaa vya kujilinda (protective gears), mfanyakazi wake,  kulingana na kazi anayofanya ili kumlinda na madhara yatokanayo na kazi anayofanya.

“Lengo la Mfuko sio tu kusajili waajiri na kupokea michango lakini pia ni kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo katika maenmeo ya kazi na ndio msingi mkuu wa seemina yetu ya leo, katika kutekeleza jukumu letu hili ni kujenga uelewa wa kutosha kwa mwajiri ili kuhakikisha kwamba tunajenga mazingira ya kuzuia ajali sehemu za kazi.” Alisema na kuongeza.
Nia ya Mfuko ni kuona tunakinda nguvu kazi ambapo tunahakikisha kwamba wafanyakazi hawa wawapo kazini hawaugui au kuumia au kufariki kutokana na kazi, alissisitiza Bw. Peter.
Alisema washiriki watapatiwa mafunzo mbalimbali yanayolenga kujenga mazingira mazuri kwa wafanyakazi wawapo kazini. “Mtaelimishwa kuhusu masuala muhimu kuhusu Mfuko kupitria mada mbalimbali zitakaziowasilishwa na wataalamu, kutekeleza vyema jukumu la kuhamasisha na kusisitiza wafanyakazi kuzingatia kanuni za kulinda usalama mahala pa kazi, masuala ya fidia kwa wafanyakazi, wanaoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.” Alifafanua.
Alisema, uwepo wa Mfuko umeleta faraja kubwa kwa waajiri na wafanyakazi ambapo leo hii, endapo Mfanyakazi atapata madhara kutokana na kazi, anao uhakika kuwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, utatoa fidia stahili kulingana na mikataba ya kazi na mwajiri husika.
“Yote haya yanawapa wafanyakazi utulivu wawapo kazini kwani wanajua kuwa lolote likitokea ipo taasisi ambayo itasimamia na kunifidia nah ii inaondoa migogoro sana sehemu za kazi.” Alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar alisema Mwajiri anao wajibu wa kumuwekea mazingira bora, salama na yana afya ili aweze kufanya kazi kwa ufanisi. “Sio tu kupewa mazingira mazuri lakini pia apewe vifaa kinga kitaalamu vinaitwa personal protective equipmentskwa kufanya hivyo utakuwa unalinda usalama wake na afya yake.” Alisema Dkt. Omar.
“Mfanyakazi anayo haki ya kumdai mwajiri wake kumpatia vifaa vya kujilinda na mwajiri haruhusiwi kumfukuza kazi au kumwadhibu mfanyakazi anayedai mazingira bora toka kwa mwajiri wake ili aweze kuwa amekingwa.” Alifafanua.
Pia alisema mfanyakazi naye anao wajibu kuvitumia vifaa vya kujikinga katika mazingira yake ya kazi kwa usahihi na wakati wote awapo kazini.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa semina hiyo, BwAlly Kinga Shamte, Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Badri East Africa Enterprises, mesema tayari kampuni yake imeanza kufaidika na kujiunga na Mfuko huo ambapo mmoja wa wafanyakazi wake, aliyepata shoti ya umeme ameweza kushughulikiwa na Mfuko na tayari anahudumiwa.
“Hii imekuwa ni kama Bima kwa wafanyakazi wetu, sisi hatushughuliki tena na madhara anayopata mfanyakazi, tulichofanya ni kujaza fomu zao za taarifa ya ajali hiyo na mara moja walianza kumshuhhulikia.” Alisema.

 
 Mshiriki akisoma machapisho yenye taarifa za WCF
 Dkt. Abdulsalaam (katikati), akifafanua baadhi ya hoja. Wengine, ni Bi. Naanjela Msangi, (Kushoto), na Bw. Faustine George
 Bi. Naanjela Msangi.
 Bw. George Faustine, Afisa Matekelezo-WCF
George Faustine, Afisa Matekelezo-WCF
  Bi. Naanjela Msangi(kulia), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kungenge
 Baadhi ya washiriki wakijadiliana jambo
 Baadhi ya washiriki wakipitia vipeperushi vyenye maelezo kuhusu kazi za Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
 Baadhi ya washiriki wa semina.
 Washiriki wakijiandikisha
 Washiriki wa semina wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wataalamu wa WCF.
 Robert Duguza, Afisa wa usalama na afya mahala pa kazi, akizungumza wakati wa semina hiyo.




Bi. Tumaini J.Kyando, Afisa Mwandamizi wa Afya na Usalama mahala pa Kazi kutoka Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio walioandaa semina hiyo, akinakili baadhi ya hoja zilizojitokeza.
Baadhi ya washiriki