HALI YA UHARIBIFU WA MISITU HANANG, MKOANI MANYARA INAKUWA KWA KASI KUBWA


Ni Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara,Teddy Athumani (wa kwanza kutoka kulia) akipitia makabrasha ya mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang kujiridhisha namna watendaji wa Halmashauri wanavyotekeleza ilani ya chama tawala.
Ni Mbunge wa jimbo la Hanang, Mkoani Manyara, Dk.Mary Nagu (wa pili kutoka kulia) akipitia taarifa ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu iliyowasilishwa kwenye mkutano huo na kisha kutaka kufahami shilingi milioni 300 zilizoagizwa kwenye mkutano wa LAC Dodoma zitalipwa lini ili vikundi vya wanawake,vijana na walemavu viweze kunufaika na kujiongezea mitaji yao.
Ni Mkuu wa wilaya ya Hanang, Sara Msafiri akisisitiza jambo kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Ni Katibu wa vikao vya Halmashauri ya wilaya ya Hanang ,Stevine Yonah (wa kwanza kutoka kushoto) akinukuu maazimio yote ya mkutano wa Baraza hilo ili watendaji waweze kutekeleza kikamilifu maazimio hayo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

Na. Jumbe Ismailly HANANG Machi,01,2018 Mazingira

KUTOKANA na hali ya uharibifu wa misitu katika wilaya ya Hanang kuwa kubwa sana,Mkuu wa wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Sara Msafiri ameziagiza kamati za maendeleo za kata kujenga utamaduni wa kujadili katika vikao vyao juu ya hali ya uhifadhi wa misitu katika maeneo yao.

Akitoa agizo hilo kwenye mkutano wa kawaida wa Baraza la kawaida la madiwani wa Halmashauri hiyo,Mkuu wa wilaya huyo aliyataja baadhi ya maeneo ya vijiji vya Lalaji.Balangida na maeneo mengine hali ya mazingira ni mbaya sana.

Kwa hiyo niwaombe kwamba kamati za maendeleo za kata mjadili na hali ya hifadhi ya misitu na ninazo taarifa za kutosha na nimejirisha wapo viongozi wengine ni wa kisiasa wanashiriki katika biashara ya kukata miti,kuchoma na kuuza mkaa.”alisisitiza Mkuu huyo wa wilaya.



Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya kupitia serikali kuu wameshatoa maagizo kwa watendaji kwamba mtu yeyote tule atakayetaka kukata miti hata kama aliupanda mwenyewe ni lazima apate kibali kutoka kwa Mkuu wa wilaya.

Hata hivyo Sara alisisitiza kwamba ni ukweli usiopingika na alioufanyia uchunguzi wa kina na kujiridhisha kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa,wakiwemo madiwani,wenyeviti wa vijiji,vitongoji na watendaji wanajihusisha na biashara ya kukata micti kuchoma mkaa na kuuza mazao hayo.
Akimpongeza Mkuu huyo wa wilaya,Mbunge wa jimbo la Hanang,Dk.Mary Nagu pamoja na kumpongeza Mkuu wa wilaya kwa jitihada zake za kulinda naa kuhifadhi mazingira,lakini aliweka bayana kuwa kama kuna jambo ambalo haliendi vizzuri katika wilaya hiyo ni suala la mazingira.

Diwani wa kata ya Hanang,mjini Peter Lori alionyesha kutoridhishwa na namna Halmashauri isivyoujali msitu wa hifadhi wa Mreru kwani kwa kipindi kirefu serikali imeitelekeza hifadhi hiyo.


Hata hivyo diwani huyo alifafanua pia kwamba inasemekana hifadhi hiyo ni mapito ya wanyama na kuhoji kwamba ni lini Mkuu wa wilaya hiyo atafikiria msitu wa hifadhi Mreru utakuwa hifadhi ya Halmashauri ya wilaya hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni