

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha kusindika Alizeti cha Mount Meru Millers kilichopo mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kwenda kukagua shughuli mbalimbali za kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti kilichopo mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa na viongozi wa Kidini kutoka Singida mara baada ya kufungua kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akifurahia jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya uzinduzi wa kiwanda hicho kikubwa cha Usindikaji wa Alizeti mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmiliki wa Kiwanda cha Mount Meru Millers Atul Mittal mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake ya uzinduzi wa kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti mkoani Singida. PICHA NA IKULU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni