MAHUSIANO KAZINI YANAKUFANYA USIJIAMINI -ANNA MAKINDA


Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu,Anne Makinda akizungumza na wanawake wa Mfuo huo leo jijin Dar es Salaam wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.


Imeelezwa kuwa mashirika mengi yamekuwa yakianguka na kukosa mweelekeo kwa sabababu ya washirika wake kuwa na mahusiano ya mapenzi wao kwa wao wawapo kazini.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti Wa bodi Wa mfuko wa Taifa Wa bima ya afya NHIF  Spika  wa bunge mstaafu Anne Makinda wakati Wa sherehe za kuadhimisha siku ya wanawake iliyofanywa na shirika hilo ofsini kwao jijini Dar es salaam.

Akizungumza na watumishi Wa NHIF Makinda amesema kuwa na mahusiano kazini yanakufanya usijiamini uwapo kazini.

"Ukiwa na mahusiano na bosi wako hata kama utafanya Kazi kwa juhudi na kupandishwa cheo itaonekana kama umepanda kwa sababu mahusiano mliyokuwa nayo,"alisema Makinda.

Makinda amewaasa wafanyakazi wa NHIF wafanye Kazi kwa uaminifu na waache makandokando.

Kwa upande wake Mkurungenzi Mkuu wa NHIFA Bernard Konga amesema shirika lao linasimamia suala zima la usawa wa kijinsia na watahakikisha wanawake wenye sifa wanapanda cheo.


Aidha Rose Gabriel ambae ni Mwenyekiti wa akina mama NHIF ametoa rai kwa wanawake kusherekea siku ya wanawake kwa kudumisha Umoja na mshikikamano

Amesema unapokuwa kazini masuala ya mahusiano uachane nayo na kufanya kazi kwa waminifu pamoja na kujituma kwa bidii.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akizungumza machache katika leo jijin Dar es Salaam wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Anne Makinda akikata keki leo wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Mhe,Anne Makinda akimlisha keki Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
 Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu Anne Makinda akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa wanawake wa (NHIF)Rose Gabriel.

 Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu,  Anne Makinda akimkabidhi zawadi wa kikombe Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Anne Makinda akilishwa keki na Mwenyekiti wa wanawake wa (NHIF)Rose Gabriel.


Baadhi ya wanawake wakiwa katika makoo makuu ya (NHIF) jijini Dar es Salaam wakisheherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila Machi 8 kila mwaka kwaajili ya kujua mchango wa mwanamke katika nafasi mbalimbali za ajira pamoja na kujua dhamani ya Mwanamke katika jamii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni