WACHIMBAJI WASUBIRIA HATMA YA MAOMBI YA LESENI MIAKA MINNE SASA BILA MAJIBU WAKATI SHERIA YA MADINI YA MWAKA 2010 NI NDANI YA SIKU 28


                                                           
Pichani ni Eneo lililotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kata ya Changaaa ambalo mmiliki wa Kampuni ya Kidee mining alilowapora wachimbaji wadogo baada ya kupewa leseni kinyemela kwa umiliki wa eneo hilo ambalo wachimbaji teyari walitafiti tokea mwaka 2012 na sasa wanatakiwa kuwa chini ya mwekezaji huyo kwa kivuli cha kikundi badala ya kampuni picha zote na mahmoud ahmad Kondoa.

Semina ikiendelea kwa Wachimbaji wadogo zaidi ya 100 wakipewa elimu ya uchimbaji sanjari na ulipaji kodi za serikali japo walipokuwa wakihoji masuala mbali mbali walikuwa wakikataliwa na maofisa madini wa ofisi ya afisa madini mkazi Dodoma hawapo pichani kama walivyokutwa na kamera yetu kwenye kata ya Changaa wilayani Kondoa.

Mbele kwenye meza ni mwenye kofia ni  diwani wa kata ya Changaa Issa Bhou na kutoka kushoto ni  Maafisa madini Affa Affa na Joshua Nduche  pamoja na katibu tarafa ya Kolo na Mwenyekiti wa kijiji cha Bubu changaa Kenyata Fonda na aliekuwa anaongea amesimama ni Afisa misitu na maliasili wilaya ya Kondoa Kasisi wakitoa semina kwa wachimbaji wa madini ya dhahabu bila kutaka kuhojiwa maswali.
                                   


                                         Na Mahmoud Ahmad Arusha
Wachimbaji wadogo wameendelea kusotea eneo lao kwa mikataba migumu inayowagawa na kuwafukuza katika maeneo yao ambapo kumekuwapo na utambulisho wa leseni tofauti tofauti katika eneo moja na kuwaacha na sintofahamu na kuelekeza lawama kwenye ofisi za Kamishna msaidizi kanda ya kati Sosthenes Masola kwa kuendelea kubariki leseni kwa kummilikisha mtu mmoja huku akitambua ana maombi halali ya wachimbaji wadogo kwenye ofisi yake bila majibu hadi sasa wakati sheria ya madini ya mwaka 2010 inasema ni ndani ya siku 28 majiubu yanakuwa teyari huku Coordness zikiksoma maombi ya wachimbaji ndani ya wizara ya madini.
Leseni hizo ambazo zimekuwa zikitolewa baada ya mh. raisi kuzuiya utoaji wa leseni hadi itakapoundwa tume zinaonekana kutaka kuwakimbiza wachimbaji katika eneo hilo kwa kigezo cha umiliki wa leseni jambo ambalo wanaziomba mamlaka kulitupia macho jambo hilo kwa uwepo wa hadaa na ukwepaji wa kodi za serikali kama ilivyobainishwa katika kikao cha mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Fallesy Kibassa na wachimbaji terehe 1\12\2017 kata ya Changaa.
Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji hao Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Juma Ramadhani Chuha amesema kuwa lengo la muongozo wa mkuu wa wilaya ya Kondoa bi Sezaria Makota kumaliza mgogoro linaonekana kugonga mwamba kwa hatua hii ya kuingia mikataba ya maduara badala ya kikundi kwa mkutano halali wa kisheria ambao ulitolewa muongozo.
Amesema badala yake amekuwa akiwaita wachimbaji kinyemela na kuwapa mikataba badala ya kukaa nao na kujadili namna nzuri ya kuainisha haki za wachimbaji na uwepo wao katika eneo lao la mgodi badala yake kumekuwepo na taratibu za kuwaondoa katika maeneo yao kwa mikataba batili ya vichochoroni badala ya kuitisha mkutano huru wa wachimbaji wote.
“kwa mujibu wa muongozo wa kamati ya ulinzi na usalama kuwataka pande zote kushirikiana na mwanasheria wa halmashauri ili kupata ufafanuzi wa kisheria jambo hilo limekiukwa na kuwa kitendawili cha kutoheshimu sheria na maamuzi ya vikao” alisisitiza Chuha
Nae Moja wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye kijiji cha BubuChangaa Mataka Iddy alisema kuwa lengo lao lilikuwa ni kufikia kumiliki eneo hilo kisheria na kulipa mapato ya serikali lakini cha kushangaza mamlaka zinatutaka tuwe chini ya mmiliki wa leseni batili ambazo ni no 005012CZ na 005013CZ ambaye wakati tunaomba eneo hilo hakuwepo wala maombi yake yalitumwa nyuma ya maombi  yetu na kupimiwa eneo na kulipia cha kushangaza sisi hatujapewa majibu hadi sasa kama tulikosa au kupata .
Amesema kuwa kimsingi wataendelea kudai haki zao hata kwa kufika kwa mh.Rais kwani wamekuwepo kisheria na wanaendelea kusotea kusimamishwa kazi kwa migogoro ilioanzishwa na wachimbaji wenzao kwa kushirikiana na mporaji wa maeneo kwa leseni mpya no 006092CZ hadi 006099CZ ambazo hapo awali kwenye kikao cha mgogoro hazikutambulishwa kwani wilaya yote imekuwa ni mali yake kwasasa katika migodi na anamiliki leseni zaidi ya 20 zisizo na tija wala ajira kwa vijana wa changaa na wilaya kwa ujumla.
Amesema kuwa pamoja na mamlaka mbali mbali walizoziendea kushindwa kutambua uhalali wa maombi yao kimsingi na majibu ya Afisa madini mkazi Kondoa Silimu Tegalile kusema wazi kuwa anamiliki leseni mbili inaonekana kuwa ni kinyume na alivyoainisha mbele ya mkuuu wa wilaya bi Sezaria Makota, jambi hili inaonekana kukidhana na leseni zinazotambulishwa kwa sasa kwenye mkataba aliotupatia wachimbaji, kwani wali zozitambulisha mbele ya mkuu wa wilaya ni leseni mbili kwenye mkataba zipo saba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni