MBUNGE MAGIGE AWASHANGAZA CCM ARUSHA

Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Arusha bi Catherine Magige ametoa kompyuta 28 kwa Jumuiya zote za chama cha mapinduzi ikiwemo Jumuiya ya wazazi,vijana,chama,na UWT zitakazosaidia chama kuendeshwa kisasa.


Akizungumza na waandishi wa Habari mkoani Arusha muda mfupi baada kikao cha ndani kilichoongozwa na Katibu mwenezi mkuu Hamphrey Polepole   bi Magige amesema kuwa kutambua umuhimu  wa kutumia  vitendea kazi vya kisasa kwa serikali ya awamu ya tano ameona vyema kutoa kompyuta hizo.


Aidha amesema kuwa kila wilaya itapatiwa kompyuta kwa kila Jumuiya ili ziweze kufanya kazi zake kisasa zaidi ambapo amesema anatambua juhudi za mheshimiwa raisi  za kutaka kazi zifanyike kisasa.
“Mimi kama mbunge nimeona changamoto waliyonayo wana CCM wenzangu hivyo nimeanza kwa kuwasaidia kompyuta kwa chama na jumuiya zake kwa maana ya Vijana, Wazazi na Wanawake ili kukifanya chama chetu cha kisasa kwa uhifadhi wa data na uandaaji wa taarifa mbalimbali” alisema Mhe Magige.

Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Hamphrey Pole Pole amesema mpango wa ukusanyaji wa mapato yote ya chama hautapitia mikononi mwa watu wakiwemo viongozi wa kata,wilaya na mkoa na badala yake zitakusanywa kwa njia ya mitandao yaani Mpesa,tigo Pesa ambapo zitafika moja kwa moja makao makuu ya chama huku akisema  kuwa mpango huo unaanza muda si mrefu.
image1.jpeg
Mhe Magige akimkabidhi kompyuta Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndg Sanare kompyuta kwaajili ya Chama cha Mapinduzi na jumuiya zake.
image2.jpeg


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni