Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka leo akiongea na wafanyakazi wa kiwanja hicho kwenye ukumbi wa mikutano wa Transit uliopo Jengo la Kwanza la abiria (TB1), ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kiutendaji. Kulia ni Afisa Rasilimali Mkuu Bi. Fatma Matimba.
Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi wa kiwanja hicho, Bw. Johannes Munanka leo alipokuwa akizungumza nao mambo mbalimbali ya kazi.
Meneja Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Vedastus Fabian (mwenye miwani mbele) akiandika mambo mbalimbali katika mkutano ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Bw. Johannes Munanka ambaye hayupo pichani.
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka akijibu maswali ya wafanyakazi wa kiwanja hicho, leo alipokutana nao katika mkutano uiliofanyika katika ukumbi wa Transit ulipo Jengo la Kwanza la abiria (TBI).
Afisa Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bi. Rachel Manyilizu akiuliza maswali kwa Kaimu Mkurugenzi wa JNIA (hayupo pichani) katika mkutano wa wafanyakazi uliofanyika kwenye ukumbi wa Transit katika jengo la Kwanza la abiria (TBI).
Afisa Usalama, Bw. Musso John, akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyoulizwa katika mkutano ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Transit uliopo katika Jengo la Kwanza la abiria (TBI).
Fundi Umeme Mwandamizi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bi Mastidia Ndyomulwango akiwasilisha hoja kwenye mkutano wa Wafanyakazi wa JNIA, ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi wake, Bw. Johannes kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji wa kazi.
Na Mwandishi Wetu
KAIMU Mkurugenzi wa Kiwanja CHA Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka amewataka wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na juhudi ili kuongeza tija na kukuza uchumi wa nchi.
Bw. Munanka alitoa kauli hiyo leo alipokutana na wafanyakazi wa JNIA, katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Transit uliopo Jengo la Kwanza la abiria (TBI), ambapo amesema wafanyakazi wasipofanya kazi kwa bidii watashindwa kuzalisha kwa ziada. Huduma kubwa inayotoa JNIA ni pamoja na kutua na kuruka kwa ndege za ndani na nje ya nchi.
Amesema wafanyakazi wasiofanyakazi kwa bidii watasababisha kuzorota kwa utoaji wa huduma kwenye Kiwanja hiki, jambo ambalo litasababisha kukimbiza abiria na wateja wengine wanaofanya shughuli zao mbalimbali kwenye kiwanja hiki, ambacho ni miongoni mwa viwanja viwili vya Kimataifa vilivyopo nchini. Kiwanja kingine cha Kimataifa ni cha Kilimanjaro (KIA).
“Ninawashukuru sana wafanyakazi wanaochapa kazi kwa bidii bila kusukumwa ingawa wengine asili ya kazi zao zinawasukuma kufanya hivyo, mfano mzuri ni waongoza ndege hawezi kutegea, tofauti na wachache waliopo katika idara nyingine wamekuwa hawana bidii ya kazi hadi wasukumwe,” amesema Bw. Munanka.
Hata hivyo, amesema wafanyakazi wote wanaosubiri kusukumwa waache mara moja na wahakikishe wanajituma wenyewe, ili kuboresha huduma zinazopatikana JNIA, ambazo zitakuwa sifa nzuri ya kuvuta wateja kutoka ndani na nje ya nchi.
“Ukiangalia katika ngazi ya meneja au wanaoingia kwenye menejimenti nao wanatakiwa kuwasimamia kwa umakini mkubwa na endapo watashindwa kufanya hivyo inanilazimu nifanye kazi za kusimamia na umeneja, ambapo sio jambo zuri litasababisha kushindwa kutekeleza majukumu mengine zaidi ya kiutendaji, hivyo ndugu zangu tuchape kazi,” amesema Bw. Munanka.
Akizungumzia vitendea kazi, Bw. Munanka ameahidi kushughulikia kwa ngazi ya JNIA ili vipatikane haraka na pia kuwasilisha Makao Makuu (Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania-TAA) vile vinavyohitaji idhini ya kuvinunua.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni