MUIGIZAJI WA HOLLYWOOD JULIA ROBERTS AACHA GUMZO MANCHESTER UNITED

Muigizaji wa Hollywood Julia Roberts ameibua mkanyanyiko baada ya jumapili kutua Old Trafford kuangilia mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza wa Manchester United na West Ham United.

Inaonekana ukaribu wa muigizaji huyo na Red Devils unaendelea baada ya kiungo wa Manchester United Paul Pogba kutupia picha kwenye Instagram jana akipigwa busu shavuni na nyota huyo Roberts.

Mchezaji huyo aliyeweka rekodi ya kusainiwa kwa dola milioni 89, ameandika maneno haya chini ya picha hiyo 'Leo nimukutana na muigizaji filamu mkubwa wa kike na mwanamke wa kipekee, nani anabahati sasa ?!'
                             Mchezaji Ander Herrera akiwa amebiga picha na Julia Roberts
       Julia Roberts akiwa amevua buti lake ili kukanyaga nyasi za dimba la Old Trafford

USAIN BOLT AZINDUA FILAMU YAKE YA 'I AM BOLT' NCHINI UINGEREZA


Mwanariadha nyota Mjamaica Usain Bolt ambaye pia ni mshindi wa medali ya dhahabu mara tisa katika michuano ya Olimpiki amezindua filamu yake ya 'I Am Bolt' nchini Uingereza.

Uzinduzi huo umefanyika ODEON Leicester Square na kuhudhuriwa na nyota kadhaa maarufu wa soka kama vile Hector Bellerin na Nacho Monreal wa Arsenal na Cesc Fabregas wa Chelsea.

Wengine waliohudhuria uzinduzi wa filamu hiyo ni Raheem Sterling, Mo Faraha, Olivier Giroud na mkewe, mchezaji wa zamani wa Arsenal Robert Pires pamoja na bondia David Haye. 
Mwanariadha Usain Bolt akiongea na waandishi wa habari waliofika katika uzinduzi wa filamu yake

RAIS WA ZAMBIA AONDOKA NCHINI KUREJEA NYUMBANI

Rais John Magufuli akiagana na Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere wakati mgeni huyo alipoondoka nchini kurejea nyumbani Novemba 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BODI YA UTALII NA SHIRIKA LA NDEGE LA ATCL WASAINI MKATABA WA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII NCHINI NA HUDUMA ZA NDEGE ZA ATCL

a1
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii TTB Bi. Devotha Mdachi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Mhandisi  Ladislaus Matindi wakisaini mkataba wa ushirikiano katika kutangaza utalii wa Tanzania na Huduma za shirika la Ndege la ATCL katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya TTB Kinondoni jijini Dar es salaam huku Mwenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  (ATCL), Emmanuel Korosso na Mwenyekiti wa Bodi ya TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo  pamoja na wanasheria wa mashirika hayo wakishuhudia tukio hilo.
a3
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Mhandisi  Ladislaus Matindi wakibadilishana hati za  mkataba wa ushirikiano katika kutangaza utalii wa Tanzania na Huduma za shirika la Ndege la (ATCL) katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya (TTB) Kinondoni jijini Dar es salaam huku Mwenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  (ATCL), Emmanuel Korosso na Mwenyekiti wa Bodi ya (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo wakishuhudia tukio hilo.
a4
Mwenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  (ATCL), Emmanuel Korosso kushoto  na Mwenyekiti wa Bodi ya (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo wakikata utepe kuzindua jarida lenye maelezo  kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utalii wa Tanzania na vivutio vyake pamoja na maelezo kuhusu huduma za usafiri wa Anga za Shirika la Ndege la Tanzania ATCL litakalopatikana pia kwenye ndege za ATCL.
a5
Mwenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  (ATCL), Emmanuel Korosso kushoto  na Mwenyekiti wa Bodi ya (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo wakionyesha jarida hilo mara baada ya kulizindua rasmi.
a6
Mwenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  (ATCL), Emmanuel Korosso kushoto akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo.
a7
Mwenyekiti wa Bodi ya (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo kulia akizungumza na waandishi katika hafla hiyo.
a8
Baadhi ya maofisa wa ATCL na TTB kutoka kulia ni Mussa Kopwe Meneja Utawala na Rasilimali Watu  kutoka  TTB , Lilian Fungamtama Ofisa Masoko wa  ATCL na Geofrey Meena Meneja Masoko TTB.
a9
Mwenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  (ATCL), Emmanuel Korosso kushoto  na Mwenyekiti wa Bodi ya (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo wakiwa katika picha ya pamoja kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii TTB Bi. Devotha Mdachi na Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL Mhandisi Ladslaus Matindi.
a10
Mwenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  (ATCL), Emmanuel Korosso kushoto  na Mwenyekiti wa Bodi ya (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo wakiwa katika picha ya pamoja kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii TTB Bi. Devotha Mdachi na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL Mhandisi Ladslaus Matindi pamoja na maofisa wengine wa TTB.
a11
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Utalii TTB pamoja na maofiza wa Wizara ya Maliasili na Utalii na TTB wakiwa katika hafla hiyo.

RAIS LUNGU WA ZAMBIA AONDOKA NCHINI

kuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange na watatu kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi John Kijazi.
kuu-1
Rais John Magufuli akiongozana na  mgeni wake, Rais Edgar Chagwa Lungu wakati mgeni huyo alipoondoka nchini kurejea nyumbani kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016.
kuu-2
Rais John Magufuli na Makamu wa Rais, Samia Suluhu wakishuudia wakati Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu akiagana na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kabla ya kuondoka nchini kurejea nyumbani Novemba 29, 2016.
kuu-3
Rais John Magufuli akiwapungia wananchi waliojitokeza kumuaga Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere wakati alipoondoka nchini kurejea nchini Novemba 29, 2016. Wengine pichani ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN ASHIRIKI DHIFA YA CHAKULA YA EDGA LUNGU RAIS ZAMBIA ILIYOANDALIWA NA RAIS MAGUFULI

zif1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) Rais wa Zambia Edga Lungu,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa Rais wa Zambia jana,katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.]28/11/2016.
zif2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta na Rais wa Zambia Edga Lungu wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam jana,[Picha na Ikulu.]28/11/2016.
zif4
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiagana na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kumalizika hafla ya dhifa ya chakula cha jioni iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,iliyoandaliwa kwa Rais wa Zambia Edga Lungu akiwa nchini kwa ziara ya siku tatu, [Picha na Ikulu.]28/11/2016.
zif6
Rais wa Zambia Edga Lungu akisalimiana na Makamo wa Rais Mstaafu wa   Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Mohamed Gharib Bilali wakati wa hafla ya dhifa ya chakula cha jioni iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,Rais Lungu yupo nchini  kwa ziara ya siku tatu, [Picha na Ikulu.]28/11/2016.
zif5
Rais wa Zambia Edga Lungu akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati wa hafla ya dhifa ya chakula cha jioni iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,Rais Lungu yupo nchini  kwa ziara ya siku tatu, [Picha na Ikulu.]28/11/2016.

MHE. POSSI: JAMII IWASHIRIKISHE WATU WENYE ULEMAVU KATIKA FURSA ZOTE ZA MAENDELEO

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi  akizungumza na baadhi ya watu wenye ulemavu (hawapo pichani) na watendaji wa Serikali juu ya umuhimu wa kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli za maendelea wakati wa ziara yake Wilayani Peramiho mkoa wa Ruvuma Novemba, 2016.
 Baadhi ya watu wenye ulemavu wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao alipotembelea kituo cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha Peramiho Disabled Persons Action(PEDIPA) wakati wa ziara yake Peramiho. 
 Mhazini wa kikundi cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha Peramiho Disabled Persons Action (PEDIPA) Mwl.Elswida Charles akimkabidhi risala ya kikundi hicho kwa  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi Peramiho Ruvuma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi   akimkabidhi Mwenyekiti wa PEDIPA Bw.Pius S.Kayombo Kiti Mwendo ili kumsaidia katika shughuli zake za kila siku.
 Mwenyekiti wa PEDIPA Bw.Pius S.Kayombo akiwa katika zoezi la kutumia kiti mwendo alichokabidhiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi alipotembelea kituo hicho Peramiho Ruvuma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi  akikabidhi mashine ya kushonea nguo  kwa Mhazini wa kikundi cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha PEDIPA Mwl.Elswida Charles wakati wa ziara yake kituoni hapo Wilayani Peramiho mkoa wa Ruvuma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi  akitoa mafuta maalum ya ngozi kwa mmoja wa washiriki wa wajumbe wa kikundi cha PEDIPA wakati wa ziara yake Ruvuma
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na Bi. Cholastika Haule ambaye ni mlemavu wa viungo mara baada ya kumalizika kwa ziara yake Wilayani Peramiho Mkoa wa Ruvuma. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na.Mwandishi Wetu
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameiasa jamii kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli zote za maendeleo ili kusaidia kuwainua na kuondokana na dhana ya utegemezi na kuwakwamua kiuchumi.
Dkt.Possi ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Wilaya za Mbinga, Songea Vijijini na Nyasa mkoani Ruvuma ambapo alitembelea Shule zenye kuhudumia watu wenye mahitaji maalum za Songea Boys, Luhira, Huruma na Kituo cha Kulelea wenye ulewavu cha Peramiho Disabled Persons Action (PEDIPA) na Kituo cha kulele wazee na wenye ukoma cha Nge Wilayani Nyasa.
Katika ziara hiyo Mhe.Possi alibaini changamoto nyingi za watu wenye ulemavu na kuishauri jamii namna pekee ya kutatua changamoto wanazokabiliana nazo ni jamii kuona umuhimu wa kuwashirikisha watu hao katika mipango yote ya maendeleo.
“Halmashauri ziandae mipango ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kuweza kushiriki kikamilifu katika kujitafutia kipato na hii itasaidia kuondokana na hali ya utegemezi na kuondoa mitazamo hasi juu ya watu wenye ulemavu kuwa hawawezi” .Alisema Mhe.Possi.
Waziri Possi alisisitiza kuwa ni lazima Halmashauri ziwe na ubunifu wa miradi ya maendeleo itakayo walenga watu wenye ulemavu, “Ni vyema sasa kuwe na jitihada za makusudi za kuunda miradi maalum kwa ajili ya kuwapa nafasi za ushiriki ili kujitafutia vipato na kuyakabili mazingira yao, ikumbukwe wakina mama waliachwa nyuma kwa muda mrefu ila baada ya kupaza sauti zao tunaona sasa wanasikika hivyo hivyo iwe kwa watu wenye ulemavu” Alisitiza Dkt.Possi.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa Dkt.Osca Albano alisisitiza kuyapokea maelekezo yote ya Naibu Waziri Mhe.Possi kwa vitendo na kumhakikishia kuwa Wilaya yao itakuwa mstari wa mbele katika kulitekeleza hilo.
 “Sisi tunafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na Halmashauri hivyo ni vyema tukalichukua hilo kuangalia namna tunavyoweza kuliweka katika mipango yetu yote ya maendeleo ili kuwasaidia na kufikia lengo la serikali,” alisema Dkt. Albano.
Nae Katibu Tawala Wilaya ya Songea Bw. Edmund Siame aliomba halmashauri zote ziwe zinatoa mrejesho mapema juu ya maagizo yanayotolewa na viongozi wa juu huku Mwalimu Elswida Charles anayehudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum akimweleza Dkt. Possi kuwa watu wenye ulemavu wanafarijika kutokana na jitihada anazofanya kuwainua watu wenye ulemavu.

PROFESA MUHONGO, WAZIRI WA NISHATI ZAMBIA WAKUTANA KUZUNGUMZIA BOMBA LA TAZAMA

 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akijadiliana jambo na Waziri wa Nishati wa Zambia, David Mabumba (kushoto) na Mkurugenzi kutoka Bomba la Mafuta la TAZAMA, D. Legge (kulia).
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia), na Waziri wa Nishati wa Zambia, David Mabumba wakifurahia jambo mara baada ya mazungumzo baina yao yaliyofanyika Ofisini kwa Waziri Muhongo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) na Waziri wa Nishati wa Zambia, David Mabumba (wa tatu kutoka kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe ulioambatana na Waziri Mabumba. Wa Tatu kutoka Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu, Profesa James Mdoe.
 Waziri wa Nishati wa Zambia, David Mabumba (kushoto) akimuaga Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kushoto) baada ya kikao chao kilichofanyika ofisini kwa Waziri Muhongo. Wa pili kutoka Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa James Mdoe akiagana na Mkurugenzi kutoka Bomba la TAZAMA, D. Legge.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia) akizungumza na Waziri wa Nishati wa Zambia David Mabumba (wa tatu kutoka kulia) na Ujumbe wake, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Waziri wa Nishati wa Zambia, David Mabumba na Ujumbe wake (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Na Veronica Simba.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati wa Zambia, David Mabumba, wamekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuboresha Bomba la Mafuta la TAZAMA ili liweze kuwanufaisha wananchi wa Tanzania na Zambia kama ilivyokusudiwa.

Mazungumzo yao yaliyofanyika mapema leo, ofisini kwa Waziri Muhongo jijini Dar es Salaam, ni kufuatia makubaliano ya marais wa nchi husika, Dk John Magufuli na Edgar Lungu; kuhusu kuboresha zaidi Bomba la TAZAMA na Reli ya TAZARA.

Marais Magufuli na Lungu, walifikia makubaliano hayo jana katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ikulu ya Dar es Salaam ambayo ni mojawapo ya shughuli mbalimbali zilizopangwa katika ratiba ya ziara ya siku Tatu (3) ya Rais Lungu iliyoanza nchini Jumapili, Novemba 21 mwaka huu. 

Waziri Mabumba ambaye alifuatana na Ujumbe wa Viongozi na Maafisa waandamizi kutoka TAZAMA na wizarani kwake; aliafiki mapendekezo yaliyotolewa na Waziri Muhongo kuhusu namna pande hizo mbili zitakavyoshirikiana katika utekelezaji wa agizo la Marais wao ambayo ni pamoja na wataalam wa pande zote kukutana na kufanya majadiliano pamoja na kufanya ziara kukagua utendaji kazi wa Bomba hilo.

Aidha, Mawaziri hao walijadiliana kuhusu namna ambavyo Zambia itanufaika na gesi asilia iliyogunduliwa Kusini mwa Tanzania. 


Kikao hicho pia, kilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini – Tanzania, akiwamo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa James Mdoe.

MANUNUZI YA PAMOJA KUPITIA GPSA: SERIKALI YAOKOA BILIONI MOJA KWENYE MAGARI

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Jacob Kibona akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Kitabu cha wageni chenye nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo wenye mamlaka ya kusambaza vitabu hivyo na nyaraka mbalimbali za serikali zenye nembo hiyo kwa taasisi za umma kwa lengo la kulinda uhalisia wa nembo ya serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.

Na Barnabas Lugwisha
Serikali kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) hivi karibuni imeokoa shilling bilioni 1.3 baada ya wakala hiyo kununua kwa pamoja magari 392 katika mpango wa serikali wa manunuzi ya pamoja.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bw Jacob Kibona, amewaambia Waandishi wa Habari jana kuwa fedha hizo zimeokolewa na serikali baada ya kununua magari 392 kwa pamoja kwa Sh. bilioni 56.1 badala ya shilingibilioni 58.1 iwapo kila taasisi ingenunua magari yake.
“Kwa kweli huu mpango wa manunuzi yapamoja ni mpango mzuri sana ambao unaiwezesha serikali kuokoa fedha nyingi,” Alisema
Alisema fedha zilizookolewa zitaiwezesha serikali kufanya shughuli nyingine za maendeleo ya ummana kama vile kuboresha miundombinu ya barabara, huduma za afya na elimu.
 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Jacob Kibona akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) faili lenye nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo wenye mamlaka ya kusambaza mafaili hayo kwa lengo la kulinda uhalisia wa nembo ya serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.

Amesema taasisi yake pia katika kipindi cha Julai hadi Oktobamwaka huu, imezikabidhi taasisi za serikali magari ya aina mbalimbali yapatayo 136.

Alisema katika kuhakisha kwamba wanapunguza gharama katika manunuzi, wamekuwa wakinunua bidhaa kutoka kwa wazalishaji moja kwa moja ila inaposhindikana kutokana na sera za makampuni makubwa kuwa na mawakala wa usambazaji wamekuwa wakinunua kwa mawakala hao kwa makubaliano maalum ya kupunguza bei.
Alisema kuwa kazi nyingine muhimu ya taasisi yake ni kugomboa mizigo kupitia bandarini , viwanja vya ndege na mipakani kwa niaba ya serikali ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita waligomboa mizigo yenye thamani ya Shlingi bilioni 62.7.

Alisema mizigo hiyo ilikuwa ni pamoja na vifaa vya mkongo wa taifa, vifaa vya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Wizara yaMali asili na utalii.
 
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Jacob Kibona akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Kitabu cha wageni chenye nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo wenye mamlaka ya kusambaza vitabu hivyo na nyaraka mbalimbali za serikali zenye nembo hiyo kwa taasisi za umma kwa lengo la kulinda uhalisia wa nembo ya serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.

Aliongeza kuwa kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu pia walikomboa vifaa mbalimbali vya serikali zikiwamo ndege mbili zilizonunuliwa na serikali kutoka Canada aina ya Bombadier vyote vikiwa na thamani ya Shilingi bilioni 100.97.

Alisema GPSA ina huduma za kuhifadhi vifaa kwa ajili ya taasisi za serikali, kwa kuwa wao wana maghala makubwa katika mikoa karibu yote .

“Hata mkoani Kagera baada ya maafa ya tetemeko la ardhi, maghala yetu yanayotumika kuhifadhi vifaa mbalimbali viliyotolewa kama misaada,”

Pia wana jukumu la kutoa huduma ya mafuta kwa magari yaserikali na kwamba kwamba hadi sasa wamefanikiwa kusimika mfumo wa usimamizi wa mafuta kwa matumizi ya ya serikali na kwamba mfumo huo unaendelea kupanuliwa ili uzifikie taasisi nyingi za umma.
Alizishauri taasisi za umma kuzingatia sheria za manunuzi kwa lengo la kutoa huduma bora na kwa kuhakikisha kuwa vifaa na huduma zinazopatikana zinazingatia thamani halisi ya fedha zinazotumika

KINANA AKUTANA NA UJUMBEA WA CPC YA CHINA

 Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya Mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo (Wakwanza kushoto),  alipokutana naye na kufanya mazungumzo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam. Bo na ujumbe wake wapo katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Mapinduzi. Wapili ni Kaimu Balozi wa China hapa Nchini, Gou hao Domg. Na walioketi kulia, ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na Katibu wa NEC, Sisa na Ushorikiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chama.
 KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman akimsalimia  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo kabla ya kuanza mazungumzo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam. Bo na ujumbe wake wapo katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Mapinduzi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Kaimu Nalozi wa China hapa nchini, Gou Hao Dong, alipowasili katika ukumbi wa Sekretarieti kwa ajili ya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo (katikati)
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akijiandaa kukaa tayari kwa mazungumzo na Jia Bo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alipowasili ukumbini. Madabida ndiye Mwenyeji wa ujumbe huo wa China
 KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman akiiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo katika picha ya pamoja na ujumbe wa CCM na CPC, baada ya mazungumzo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam. Bo na ujumbe wake wapo katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Mapinduzi. 
 KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman akiagana na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Hao Dong, baada ya mazungumzo.
Balozi wa China hapa nchini, Gou Ho Dong akiagana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chana baada ya mazungumzo hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, ramadhani Madabida.