Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) Rais wa Zambia Edga Lungu,Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Makamo wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakisimama
wakati wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni
kilichoandaliwa kwa Rais wa Zambia jana,katika ukumbi wa Ikulu Jijini
Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.]28/11/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta na Rais wa Zambia Edga Lungu wakati
wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Ikulu
Jijini Dar es Salaam jana,[Picha na Ikulu.]28/11/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiagana na
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
baada ya kumalizika hafla ya dhifa ya chakula cha jioni iliyofanyika
jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,iliyoandaliwa kwa
Rais wa Zambia Edga Lungu akiwa nchini kwa ziara ya siku tatu, [Picha na
Ikulu.]28/11/2016.
Rais wa Zambia Edga Lungu
akisalimiana na Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilali wakati wa hafla ya dhifa ya chakula
cha jioni iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es
Salaam,Rais Lungu yupo nchini kwa ziara ya siku tatu, [Picha na Ikulu.]28/11/2016.
Rais wa Zambia Edga Lungu
akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee
Ali Hassan Mwinyi wakati wa hafla ya dhifa ya chakula cha jioni
iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,Rais
Lungu yupo nchini kwa ziara ya siku tatu, [Picha na Ikulu.]28/11/2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni