MAKONDA APIGA MARUFUKU BIASHARA YA SAMAKI KANDOKANDO YA BARABARA

Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar,Paul Makonda amepiga marufuku biashara ya samaki kandokando ya barabara inayoelekea kivukoni na soko la samaki la feri baada ya wafanyabishara wa feri kulalamika kwa mkuu wa mkoa huyo kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakwepa kodi.

Awali Makonda aliambiwa na wafanyabiashara hao kuwa soko hilo linakosa wateja kutokana na kushindwa kufikiwa na wateja ambao hununua samaki au bidhaa nyengine kandokando ya barabara na kusababisha wateja kutofika sokoni humo.

Wakati huo huo Makonda amesikitishwa na kitendo cha wakuu wa idara mbalimbali kushindwa kukamilisha miradi kwa wakati kwa kisingizo cha kutopata fedha za bajeti ya serikali kuu ikiwa wangeweza kubuni miradi itakayowaingizia fedha.

RC Makonda alisema kuwa hatakubaliana na watendaji wa namna hiyo kwani hurudisha maendeleo nyuma.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na viongozi na watendaji wa wilaya ya Ilala katika ukumbi wa Anatoglo leo jijini Dar es salaam.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala,Edward Mpogolo akizungumza macheche katika ukumbi wa Anatoglo leo jijini Dar es salaam.
 Viongozi na watendaji wa wilaya ya Ilala wakimsikiliza  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ukumbi wa Anatoglo leo jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Feri ambapo pia alisikiliza  kero zao leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Mkonda akikagua madarasa ya mradi wa MEMS 11 Pugu Station Sekondari leo jijini Dar es Salaam.
 Mnada wa samaki katika Soko la Feri ukiendelea. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.












Hakuna maoni:

Chapisha Maoni