Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Hebron Mwakagenda akitoa mafunzo kuhusu katiba ya zamani pamoja na katiba mpya kwa vijana kutoka wilaya zote za jiji la Dar es Salaam leo. (Picha na Geofrey Adroph)
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na historia ya mchakato huo kwa vijana wa wilaya zote za jiji la Dar Es Salaam.
Katibu Mtendaji wa TYVA, Saddam Khalfan akitoa ufafanuzi kuhusu shirika hilo na madhumuni ya mjadala wa katiba na vijana uliyofanyika katika ukumbi wa Blue Pearl jijini Dar Es Salaam
Mbunge wa Viti Maalumu, (CUF), Riziki Lulida akizungumzia changamoto wanazozipata kama wabunge wenye ulemavi katika katiba pamoja na kutoa maoni kuhusu uundwaji wa katiba mpya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni