Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana
na Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu kwenye uwanja wa ndege wa
Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016. Wapili
kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange na watatu
kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi John Kijazi.
Rais John Magufuli akiongozana na
mgeni wake, Rais Edgar Chagwa Lungu wakati mgeni huyo alipoondoka
nchini kurejea nyumbani kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage
Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016.
Rais John Magufuli na Makamu wa Rais,
Samia Suluhu wakishuudia wakati Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu
akiagana na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa ndege wa Julius
Kambarage Nyerere kabla ya kuondoka nchini kurejea nyumbani Novemba 29,
2016.
Rais John Magufuli akiwapungia wananchi
waliojitokeza kumuaga Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu kwenye uwanja
wa ndege wa Julius Nyerere wakati alipoondoka nchini kurejea nchini
Novemba 29, 2016. Wengine pichani ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu na
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni