RC GAMBO ABAINI UBADHIRIFU MACHINJIO YA MANYARA RANCH


     Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(katikati) akiwasili kwenye Machinjio ya Manyara Ranch kukagua mradi huo uliopata fedha za wafadhili zaidi ya Tsh Mil 400.

      Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kati mbele)  akipokea taarifa ya Machinjio ya Manyara Ranch toka kwa Meneja wa AWF Ndg. Fidelisi Ole Kashe(kulia)

      Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (pili kushoto) akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wilaya ya Monduli baada ya kubaini ubadhirifu wa Fedha katika wa Mradi wa Machinjio.

    Huu ndio muonekano wa Machinjio ya mManyara Ranch

  Malaigwanani wa Kimaasai Wilayani Monduli wakimsimika Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyekaa kwenye Kigoda) kuwa Laigwanani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Esilalei.


                                 Na Mahmoud Ahmad, Monduli
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoani Arusha(TAKUKURU) kuhakikisha inawakamata na kuwafikisha mahakamani wale wote waliokula fedha zaidi ya shilingi milioni 448.9 za mradi wa machinjio uliopo ndani ya shamba la Manyara Ranch lililopo wilayani Monduli Mkoani Arusha.
 Gambo alisema hayo mara baada ya kutembelea machinjio hayo ya kisasa yaliyopo ndani ya shamba hilo la ekari 44,930 na kuelezwa kuwa mradi huo ulianza mwaka 2009 na hadi sasa ulikuwa haujamalizika.

 Alisema inasikitisha kuona mradi toka mwaka 2009 zaidi ya miaka saba haujakamilika pamoja na kwamba fedha zaidi ya shilingi milioni 448.9 zilitolewa ikiwa ni gharama za ujenzi na ujenzi wa jengo la machinjio uligharimu zaidi ya shilingi milioni 223.5 na ununuzi wa vifaa vingine vya kisasa kwa ajili ya machinjio zilitolewa zaidi ya shilingi milioni 225.4
 Mkuu huyo alisema kuwa fedha zimetolewa na wafadhili ambao ni USAID kupitia shirika la African Wildlife Foundation(AWF) lakini zimeliwa na wajanja na mradi ukwama kufanya kazi kwa miaka hiyo yote na wahusika wako na wengine wako wizara ya mifugo na kilimo hilo halitavumiliwa kamwe lazima hatua zichukuliwe haraka.

 Alisema TAKUKURU inapaswa kuchukua hatua kwa kuwasaka wale wote waliohusika kukwamisha mradi huu kwa kutafuna fedha hizo na kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola kujibu mashitaka.

  ‘’Haiwezekani watu wanakula fedha za wafadhili ambao wana nina nzuri na nchi halafu tunawaacha hilo sio kwa serikali hii ya awamu ya tano  inayoongozwa na Rais Dkt John  Magufuli’’

 ‘’Lazima wale wote waliokula fedha za wafadhili wanapaswa kukamatwa mara moja na hiyo nawaachia Takukuru ndani ya siku chache zijazo nahitaji majibu kuwa wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yao’’ alisema Gambo

 Meneja wa AWF, Fidelis Ole Kashe alisema lengo la kujengwa kwa machinjio katika shamba hilo ni pamoja na kupanuaa wigo wa vyazo vya mapato yanayotokana na kuuza mifugo na nyama iliyo bora katika kiwanda hicho na kutoza ushuru wa pango kutoka kwa mwekezaji atayefanikiwa kuendesha machinjio hayo.

 Sambamba na hilo Kashe alisema kuwa kiwanda hicho cha machinjio kitatoa soko la kuuza mifugo na nyama katika vijiji vinavyozunguka machinjio na pia ajira itatolewa kw wananchi ikiweka kipaumbele kwa jamii zilizo jirani na machinjio hayo.

Kashe alisema kuwa mapungufu yaliyopo katika mradi huo ni pamoja na kutolewa fedha nyingi lakini hadi sasa mradi huo kushindwa kukamilika, kukosekana kwa mwekezaji,vifaa vilivyotumika kujenga havina ubora, mradi haukuwekewa mipango endelevu na wafadhili kusitisha kutoa fedha tena kumalizia mradi huo wakati fedha zilizotolewa hazina maelezo zilitumikaje.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni