Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akizungumza na baadhi ya watu wenye ulemavu (hawapo pichani) na
watendaji wa Serikali juu ya umuhimu wa kuwashirikisha watu wenye
ulemavu katika shughuli za maendelea wakati wa ziara yake Wilayani
Peramiho mkoa wa Ruvuma Novemba, 2016.
Baadhi
ya watu wenye ulemavu wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza nao alipotembelea kituo cha kulelea watu wenye mahitaji
maalum cha Peramiho Disabled Persons Action(PEDIPA) wakati wa ziara yake Peramiho.
Mhazini wa kikundi cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha Peramiho Disabled Persons Action (PEDIPA)
Mwl.Elswida Charles akimkabidhi risala ya kikundi hicho kwa Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi Peramiho Ruvuma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akimkabidhi Mwenyekiti wa PEDIPA Bw.Pius S.Kayombo Kiti Mwendo ili kumsaidia katika shughuli zake za kila siku.
Mwenyekiti
wa PEDIPA Bw.Pius S.Kayombo akiwa katika zoezi la kutumia kiti mwendo
alichokabidhiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye
Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi alipotembelea kituo hicho Peramiho
Ruvuma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akikabidhi mashine ya kushonea nguo kwa Mhazini wa kikundi cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha PEDIPA Mwl.Elswida Charles wakati wa ziara yake kituoni hapo Wilayani Peramiho mkoa wa Ruvuma.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akitoa mafuta maalum ya ngozi kwa mmoja wa washiriki wa wajumbe
wa kikundi cha PEDIPA wakati wa ziara yake Ruvuma
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akisalimiana na Bi. Cholastika Haule ambaye ni mlemavu wa viungo
mara baada ya kumalizika kwa ziara yake Wilayani Peramiho Mkoa wa
Ruvuma. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Na.Mwandishi Wetu
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameiasa jamii
kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli zote za maendeleo ili
kusaidia kuwainua na kuondokana na dhana ya utegemezi na kuwakwamua
kiuchumi.
Dkt.Possi ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Wilaya za Mbinga, Songea Vijijini na Nyasa mkoani Ruvuma ambapo alitembelea Shule zenye kuhudumia watu wenye mahitaji maalum za Songea Boys, Luhira, Huruma na Kituo cha Kulelea wenye ulewavu cha Peramiho Disabled Persons Action (PEDIPA) na Kituo cha kulele wazee na wenye ukoma cha Nge Wilayani Nyasa.
Katika ziara hiyo Mhe.Possi alibaini changamoto
nyingi za watu wenye ulemavu na kuishauri jamii namna pekee ya kutatua
changamoto wanazokabiliana nazo ni jamii kuona umuhimu wa kuwashirikisha
watu hao katika mipango yote ya maendeleo.
“Halmashauri
ziandae mipango ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kuweza kushiriki
kikamilifu katika kujitafutia kipato na hii itasaidia kuondokana na hali
ya utegemezi na kuondoa mitazamo hasi juu ya watu wenye ulemavu kuwa
hawawezi” .Alisema Mhe.Possi.
Waziri
Possi alisisitiza kuwa ni lazima Halmashauri ziwe na ubunifu wa miradi
ya maendeleo itakayo walenga watu wenye ulemavu, “Ni vyema sasa kuwe na
jitihada za makusudi za kuunda miradi maalum kwa ajili ya kuwapa nafasi
za ushiriki ili kujitafutia vipato na kuyakabili mazingira yao,
ikumbukwe wakina mama waliachwa nyuma kwa muda mrefu ila baada ya kupaza
sauti zao tunaona sasa wanasikika hivyo hivyo iwe kwa watu wenye
ulemavu” Alisitiza Dkt.Possi.
Aidha
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa Dkt.Osca Albano alisisitiza
kuyapokea maelekezo yote ya Naibu Waziri Mhe.Possi kwa vitendo na
kumhakikishia kuwa Wilaya yao itakuwa mstari wa mbele katika
kulitekeleza hilo.
“Sisi
tunafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na Halmashauri hivyo ni vyema
tukalichukua hilo kuangalia namna tunavyoweza kuliweka katika mipango
yetu yote ya maendeleo ili kuwasaidia na kufikia lengo la serikali,”
alisema Dkt. Albano.
Nae
Katibu Tawala Wilaya ya Songea Bw. Edmund Siame aliomba halmashauri
zote ziwe zinatoa mrejesho mapema juu ya maagizo yanayotolewa na
viongozi wa juu huku Mwalimu Elswida Charles anayehudumia wanafunzi
wenye mahitaji maalum akimweleza Dkt. Possi kuwa watu wenye ulemavu
wanafarijika kutokana na jitihada anazofanya kuwainua watu wenye
ulemavu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni