Ndege ya abiria ikiwana watu 81,
wakiwemo wachezaji wa timu ya Chapecoence ya Brazil imeanguka katika
mji wa Medellin nchini Colombia.
Ndege hiyo imeanguka wakati
ikikaribia mji huo baada ya kupata hitilafu katika mfumo wa umeme,
ambapo taarifa zinasema watu sita wamenusurika kifo.
Wachezaji hao wa timu ya Chapecoence
walikuwa wanaenda katika mchezo wa fainali ya Copa Sudamericana,
dhidi ya timu ya Medellin ya Atletico Nacional.
Viongozi na wachezaji wa timu ya Chapecoence wakiwa kwenye ndege hiyo kabla ya kuanguka
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni