Mwanariadha nyota Mjamaica Usain
Bolt ambaye pia ni mshindi wa medali ya dhahabu mara tisa katika
michuano ya Olimpiki amezindua filamu yake ya 'I Am Bolt' nchini
Uingereza.
Uzinduzi huo umefanyika ODEON
Leicester Square na kuhudhuriwa na nyota kadhaa maarufu wa soka kama
vile Hector Bellerin na Nacho Monreal wa Arsenal na Cesc Fabregas wa
Chelsea.
Wengine waliohudhuria uzinduzi wa
filamu hiyo ni Raheem Sterling, Mo Faraha, Olivier Giroud na mkewe,
mchezaji wa zamani wa Arsenal Robert Pires pamoja na bondia David
Haye.
Mwanariadha Usain Bolt akiongea na waandishi wa habari waliofika katika uzinduzi wa filamu yake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni