Rapa nyota nchini Marekani Kanye West amelazwa hospitali kwa muda kwa usalama wake baada ya kuchanganyikiwa kiakili.
Chanzo kimoja kimesema rapa huyo kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa madaktari wa akili katika kituo cha UCLA Medical Center huko Los Angeles na kusitisha ziara yake ya muziki ya Saint Pablo.
Rafiki zake wameieleza DailyMail.com kuwa kuchanganyikiwa kwa Kanye kunatokana na matatizo ya ndoa yake na Kim Kardashian, kuvunja urafiki na Jay Z na kumuonea wivu Beyoncé.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni