Kaimu 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) 
Jacob Kibona akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Kitabu 
cha wageni chenye  nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo 
wenye mamlaka ya kusambaza  vitabu hivyo  na nyaraka mbalimbali za 
serikali zenye nembo hiyo kwa taasisi za umma kwa lengo la kulinda 
uhalisia wa nembo ya serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.
Na Barnabas Lugwisha
Serikali
 kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) hivi karibuni 
imeokoa shilling bilioni 1.3 baada ya wakala hiyo kununua kwa pamoja 
magari 392 katika mpango wa serikali wa manunuzi ya pamoja.
Kaimu 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bw Jacob Kibona, amewaambia 
Waandishi wa Habari jana kuwa fedha hizo zimeokolewa na serikali baada 
ya kununua magari 392 kwa pamoja kwa Sh. bilioni 56.1 badala ya 
shilingibilioni 58.1 iwapo kila taasisi ingenunua magari yake.
“Kwa kweli huu mpango wa manunuzi yapamoja ni mpango mzuri sana ambao unaiwezesha serikali kuokoa fedha nyingi,” Alisema
Alisema
 fedha zilizookolewa zitaiwezesha serikali kufanya shughuli nyingine za 
maendeleo ya ummana kama vile kuboresha miundombinu ya barabara, huduma 
za afya na elimu.
Kaimu 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Jacob 
Kibona akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) faili lenye 
nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo wenye mamlaka ya 
kusambaza mafaili hayo kwa lengo la kulinda uhalisia wa nembo ya 
serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.
Amesema
 taasisi yake pia katika kipindi cha Julai hadi Oktobamwaka huu, 
imezikabidhi taasisi za serikali  magari  ya aina mbalimbali  yapatayo 
136.
Alisema
 katika kuhakisha kwamba wanapunguza gharama katika manunuzi, wamekuwa 
wakinunua bidhaa kutoka kwa wazalishaji moja kwa moja ila 
inaposhindikana kutokana na sera za makampuni makubwa kuwa na mawakala 
wa usambazaji wamekuwa wakinunua kwa mawakala hao kwa makubaliano maalum
 ya kupunguza bei.
Alisema
 kuwa kazi nyingine muhimu ya taasisi yake ni kugomboa mizigo kupitia 
bandarini , viwanja vya ndege na mipakani kwa niaba ya serikali ambapo 
kwa mwaka wa fedha uliopita waligomboa mizigo yenye thamani ya Shlingi 
bilioni 62.7.
Alisema
 mizigo hiyo ilikuwa ni pamoja na vifaa vya mkongo wa taifa, vifaa vya 
Mamlaka ya Mapato Tanzania na Wizara yaMali asili na utalii.
Kaimu 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), 
Jacob Kibona akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Kitabu 
cha wageni chenye nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo 
wenye mamlaka ya kusambaza vitabu hivyo na nyaraka mbalimbali za 
serikali zenye nembo hiyo kwa taasisi za umma kwa lengo la kulinda 
uhalisia wa nembo ya serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.
Aliongeza
 kuwa kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka  huu pia 
walikomboa vifaa mbalimbali vya serikali zikiwamo ndege mbili 
zilizonunuliwa na serikali kutoka Canada aina ya Bombadier vyote vikiwa 
na thamani ya Shilingi bilioni 100.97.
Alisema
 GPSA ina huduma za kuhifadhi vifaa kwa ajili ya taasisi za serikali, 
kwa kuwa wao wana maghala makubwa katika mikoa  karibu yote .
“Hata 
mkoani Kagera baada ya maafa ya tetemeko la ardhi, maghala yetu 
yanayotumika kuhifadhi vifaa mbalimbali viliyotolewa kama misaada,”
Pia 
wana jukumu la kutoa huduma  ya mafuta kwa magari yaserikali na kwamba 
kwamba hadi sasa wamefanikiwa kusimika mfumo wa usimamizi wa mafuta kwa 
matumizi ya  ya serikali na kwamba mfumo huo unaendelea kupanuliwa ili 
uzifikie taasisi nyingi za umma.
Alizishauri
 taasisi za umma kuzingatia sheria za manunuzi kwa lengo la kutoa huduma
 bora na kwa kuhakikisha kuwa vifaa na huduma zinazopatikana 
zinazingatia thamani halisi ya fedha zinazotumika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni