BASTIAN SCHWEINSTEIGER ATWAA TUZO YA BAMBI NYUMBANI KWAO UJERUMANI


Mchezaji asiyetakiwa Manchester United, Bastian Schweinsteiger, ameshinda tuzo maalum nchini Ujerumani ijulikanayo kama BAMBI.

Licha ya kucheza michezo michache na Manchester United mwaka jana Waandaaji wa Tuzo hizo za Vyombo vya Habari wametunuku tuzo Schweinsteiger kwa mchango wake katika michezo ya kimataifa.

Schweinsteiger, 32, alistaafu kucheza soka kimataifa mwezi Agosti, akiwa ametwaa kombe la dunia na kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Euro.

                                  Kocha wa Ujerumani Joachim Low naye alitwaa tuzo ya Bambi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni