Na Mahmoud Ahmad, Arusha.
Kutokana na ombi la Lema kutaka mahakama ipitie rejeo upya la maamuzi ya mahakama kuu juu ya pingamizi la dhamana yake, upande wa Jamhuri umeweka pingamizi juu ya ombi hilo.
Akizungumza upande wakili upande wa Jamhuri Paul Kidochi aliwasilisha hoja mbili za kisheria kuweka pingamizi juu ya ombi hilo mbele ya Kaimu Jaji Sekela Moshi hapo jana.
Lakini pia alisema hoja ya pili licha kuwa ilikuwa mbinu nyingine ya kupinga ombi hilo ,alisema kwakua ilikuwa ni haki ya Lema kupatata dhamana bado muombaji hakufuata utaratibu unaotakiwa ambao ulimtaka akate rufaa na siyo kuomba mahakama.
Pia alisema kitendo cha kutokukata rufaa ni kutumia njia ya kuomba mahakama rejeo la maamuzi ya kesi hiyo ,ni kinyume na utaratibu na kama mahakama itatupilia mabali pingamizi hilo itakuwa itakuwa imeharibu mfumo mzima wa uendeshaji wa kesi hiyo.
"Mheshimiwa Jaji kama utaruhusu mfumo huo basi kila mtu atakuwa anaandika barua na si kukata rufaa." alisema wakili wa serikali.
Kwa upande wa wa wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala ameiambia mahakama kuwa nini tafsiri la pingamizi la awali,ameiambia mahakama kuwa pingamizi hilo halina mashiko kisheria huku akitaja kifungu cha sheria 148(6)kuwa mahakama ikitoa dhamana ni lazima itoe na masharti kama haijaweka imevunja haki yake kisheria.
Kutokana na malumbano ya kisheria kati ya mawakili wa jamhuri na wale wa Lema Kaimu Jaji Sekela Cyril Moshi alitoa uamuzi huo jana hadi jumamnne ya wiki ijayo tarehe 22 novemba 2016 litakapotolewa uamuzi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni