GAMBO AANZISHA KAMPENI YA KUWAKOPESHA PIKIPIKI WAENDESHA BODABODA WA JIJI LA ARUSHA HUKU PIKIPIKI 200 ZATARAJIWA KUKOPESHWA

Image result for rc arusha gambo


Na Mahmoud Ahmad Arusha
Wadau wa maendeleo kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wametoa jumla ya pikipiki 200 zenye thamani ya Tsh.milion 400 kwa ajili ya kuwakoposha waendesha boda boda lengo likiwa ni kuweza kumiliki vyombo hivyo na kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na waendesha bodaboda wa jiji la Arusha katika ukumbi wa Golden Rose Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa lengo la kutoa mkopo kwa vijana waendesha bodaboda ni kuweza kuwasaidia kuwatoa eneo moja kwenda jingine kuacha kutumika na kuweza kumuliki vyombo hivyo vitakavyowasaidia kujikwamua kiuchumi.

Alisema kuwa mkopo watakaotoa hautakuwa na Riba na utarudishwa kwa mwaka mmoja ambapo kila kata itapata pikipiki 8 ambazo watapewa wali ambao hawana pikipiki na wanaendesha pikipiki za watu kwa makubaliano.
“Pikipiki hizi zitakabidhiwa siku ya tarehe 3 ya mwezi ujao na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuwakwamua kiuchumi vijana waendesha bodaboa kuweza kurahisisha huduma na kujukwamua kiuchumi”alisema Gambo

Katika hatua nyingene katika mkutano huo ambao uliweza kuwapata viongozi wa mpito wa chama cha waendesha boda boda jiji la Arusha(CHAWABOA)ambao wanajukumu la kuandaa na kuratibu uchaguzi wa kuwapata vijana nane kutoka kila kata ambazo ni 25 ambao watakabidhiwa pikipiki na waziri mkuu,na kuratibu uchuguzi wa viongozi kuanzia ngazi ya kata na wilaya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni