WATU 12 WAKAMATWA NA POLISI ISRAELI KWA TUHUMA ZA KUWASHA MOTO


Polisi nchini Israeli imewakamata watu 12 kwa tuhuma za kuwasha moto wa nyika uliounguza maeneo kadhaa ya mji wa Haifa kwa siku nne.

Vikosi vya zimamato vimefanikiwa kuudhibiti moto huo kaskazini mwa mji wa Haifa, ambao wakazi wake wapatao 80,000 waliagizwa kuuhama.

Hata hivyo maafisa wa zimamoto wamesema kuwa bado kuna moto midogo midogo inayoendelewa kuzimwa katika maeneo tofauti.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni