TIMU YA ARSENAL NA PARIS ST-GERMAIN ZATOSHANA NGUVU


Timu ya Arsenal imeshindwa kukwea na kuongoza kundia A katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutoka sare ya goli 1-1 na Paris St-Germain katika dimba la Emirates.

Ilionekana kama Arsenal wataweza kuongoza kundi hilo licha ya kufungwa goli la mapema lililofungwa kwa kuteleza na Edinson Cavani akiunganisha krosi ya Blaise Matuidi.

Olivier Giroud alifunga kwa mkwaju wa penati na kusawazisha goli, na kisha baadaye Marco Verratti akajifunga, kabla ya Alex Iwobi naye kujifunga kwa mpira wa kichwa uliopigwa na Lucas Moura.
                 Edinson Cavani akiteleza na kufunga goli la kwanza katika mchezo huo

 Alex Iwobi akiwa anashangaa baada ya kujifunga huku kipa wao akiwa amelala chini

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni