Timu ya Celtic imeondolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Barcelona ikiongoza kundi C katika michuano hiyo.
Katika mchezo huo Lionel Messi alifunga goli la kwanza kufuatia pasi ya kiufundi kutoka kwa Neymar, na kisha baadaye kipa Craig Gordon akamnyima goli Luis Suarez.
Mchezaji Celtic Moussa Dembele alijikuta akipoteza nafasi nzuri ya kufunga kabla ya Lionel Messi kufunga goli la pili kwa mkwaju wa penati.
Lionel Messi akiachia shuti la mguu wake wa kushoto na kuandika goli la kwanza
Lionel Messi akifunga goli la pili kwa mkwaju wa penati
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni