LIVERPOOL YASHINDA HUKU IKIMPOTEZA COUTINHO ALIYEUMIA

Liverpool imefikisha michezo 11 ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyocheza bila ya kupoteza baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Sunderland lakini huenda ikawa na wakati mgumu bila mchezaji wao Philippe Coutinho aliyeondolewa uwanjani kwa machela.

Mchezaji huyo raia wa Brazil alitenguka enka yake wakati akikabiliana na Didier Ndong katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza ambacho Liverpool ilikitawala kwa asilimia 80 bila ya kufunga.

Hata hivyo Liverpool waliendelea kushambulia lango la Sunderland na alikuwa Divock Origi aliyeingia kuchukua nafasi ya Coutinho na kuifungia goli la kwanza na kisha James Milner kufunga la pili kwa mkwaju wa penati wa dakika za majeruhi.
Divock Origi akiachia shuti lililoenda na kujaa wavuni na kuifungia Liverpool goli la kwanza
Enka ya Philippe Coutinho ikiwa inaonekana kupinda baada ya kubambikiana na Didier Ndong 
Philippe Coutinho akigugumia maumivu baada ya enka yake kuumia huku refa akiwa amemshika bega

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni