Na Mahmoud Ahmad Arusha
IMEELEZWA
kuwa halmashauri nyingi hapa nchini
zinaongoza kwa kupokea rushwa kubwa kubwa huku jeshi la polisi likiongoza kwa
kupokea rushwa ndogo ndogo suala ambalo limepelekea mapambano dhidi ya rushwa
kuwa magumu.
Hayo
yameelezwa jana na Mkurugenzi wa Takukuru Valentino Mlowola wakati wa mkutano
wa mkuu mwaka wa siku 2 wa Shirikisho la mamlaka za kuzuia na kupambana na
rushwa nchi za Afrika Mashariki(EAAACA) unaofanyika jijini Arusha ambapo
unawashiriki kutoka mataifa 8 barani Afrika.
Mlowola
alisema kuwa Hadi sasa katika kipindi cha mwaka mmoja wa wameweza kuokoa zaidi
ya billion 45 za miradi mbalimbali zilizokuwa ziangukie mikononi mwa watu
wachache ambapo aliitaka jamii kutoa ushirikiano dhidi ya mapambano ya kuzuia
rushwa.
Alisema
kuwa miradi mingi inayopitia katika halmashauri nyingi hapa nchini imekuwa
ikigubikwa na rushwa na kuifanya miradi hiyo kujengwa chini ya viwango hali
inayopelekea matumizi mabaya ya fedha za umma.
Aidha
katika jeshi la Polisi alitanabaisha kuwa kumekuwa na ongezeko la kuomba na
kupokea rushwa ndogo kutoka kwa jamii hali inayosababisha wananchi kukosa imani
na kupelekea malalamiko kwa jeshi hilo.
“Waandishi
wa habari iwapo mtaona mradi wowote hauendi kwa viwango vilivyokusudiwa mtoe
taarifa kwani hivi sasa tuna maofisa wetu katika kila wilaya ambao wataweza
kufanya uchunguzi na kubaini mianya ya rushwa”alisema Mlowola
Kwa
upande wake waziri wa nchi ofisi ya Raisi Utumishi na Utawala Bora Angela Kairuki alisema kuwa serikali imeanzisha
mahakama ya mafisadi ambapo kesi kadhaa zimeanza kusikilizwa hali itakayopelekeakupunguza
kuomba na kupokea rushwa hapa nchini.
Alisema
kuwa kesi nyingi zimepelekwa katika mahakama hiyo na siku si nyingi mafanikio
ya vita dhidi ya ubadhirifu wa mali za umma utapungua kama sio kwisha kabisa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni