Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Jiji La Arusha Athmani Kihamia ametangaza kusitisha mikataba
ya wafanyakazi 66 kati ya 132 wasio na kazi za ulazima katika halmashauri hiyo
,lengo likiwa ni kubana matumizi, ambapo fedha zitakazookolewa zitaelekezwa
kwenye matumizi ya miradi ya maendeleo na ulipaji wa madeni ya nyuma.
Alisema hayo
wakati akiongea na wanahabari ofisini kwake ambapo alisema kuwa kabla hapo
alikuwa akilipa mishahara ambayo ilikuwa inaibebesha halmashauri hiyo mzigo mkubwa
na kufanya ielemewe kwa kupoteza fedha hizo ambazo zingetumika kwenye miradi ya
maendeleo na ulipaji wa madeni.
Alisema kuwa
anasimamia kubana matumizi ili kulipa madeni yenye kero na tija kama ambavyo walielekezwa na kamati za bunge na
mdhibiti mkuu wa serikali(CAG) kuhakikisha wanabana matumizi yasiyo na ulazima
ili kulipa madeni ya muda mrefu.
“Wafanyakazi
hao 132 ambao walikuwa kwenye vitengo
mbali mbali ndani ya halmashauri hiyo kati yao 66 ndio tumewapunguza kwa kuwa
kazi zao hazina umuhimu na wamekuwa mzigo hivyo ni busara kuwapunguza
kuhakikisha tunabana matumizi na kulipa madeni ya halmashauri ya nyuma”alisema
Kihamia.
Akizungumzia
tuhuma za ulipaji wa fedha za walimu 701 kiasi cha tsh. million 169 zikiwa
madeni ya walimu ambazo hazikufuata utaraatibu wa kuidhinishwa na baraza la
madiwani au kamati ya fedha na uchumi alisema kuwa fedha hizo zinatokana na
mapato ya ndani nasi lazima fedha zinazotumika kuidhinishwa na baraza au kamati
ya fedha.
“Kumekuwa na
tuhuma mbali mbali za fedha za madeni ya waalimu kutoka kwa madiwani wetu, fedha tulizowalipa waalimu kiasi cha million
169 kati ya walimu 701 hizi fedha
mchakato wake ni fedha za mapato ya ndani hazihitaji mpaka kuwepo na ukaaji wa
vikao vya baraza wala kamati”alisisitiza Kihamia.
Akawataka
wale wanaolifanya suala hilo kisiasa zaidi sio kweli kwani yeye anafuata kanuni
na taratibu katika ulipaji wa madeni ya fedha za watumishi wa umma kama
alivyowalipa walimu hao.
Akatanabaisha
kuwa katika kuhakikisha suala zima la upatikanaji wa huduma bora za Afya
halmashauri hiyo imenunua Genereta kubwa katika kituo cha Afya Levolosi ikitumia
mapato yake ya ndani jambo ambalo limerahisha utoaji wa huduma pindi umeme
unapokatika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni