Muigizaji wa Hollywood Julia Roberts
ameibua mkanyanyiko baada ya jumapili kutua Old Trafford kuangilia
mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza wa Manchester United na West Ham
United.
Inaonekana ukaribu wa muigizaji huyo
na Red Devils unaendelea baada ya kiungo wa Manchester United Paul
Pogba kutupia picha kwenye Instagram jana akipigwa busu shavuni na
nyota huyo Roberts.
Mchezaji huyo aliyeweka rekodi ya
kusainiwa kwa dola milioni 89, ameandika maneno haya chini ya picha
hiyo 'Leo nimukutana na muigizaji filamu mkubwa wa kike na mwanamke
wa kipekee, nani anabahati sasa ?!'
Mchezaji Ander Herrera akiwa amebiga picha na Julia Roberts
Julia Roberts akiwa amevua buti lake ili kukanyaga nyasi za dimba la Old Trafford
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni