Shirika la
uhifadhi wa maliasili na mazingira Duniani(WWF)kwa kushirikiana na wakala wa
misitu Tanzania(TFS) wamefanya mafunzo kwa maofisa misitu waliopo mipakani na
maafisa Kilimo pamoja na idara ya forodha kwa lengo la kudhibiti utoroshwaji wa
mazao ya misitu katika mipaka inayotenganisha nchi na
nchi.
Semina hiyo
ya siku tatu inayofanyika jijini Arusha na kuzishrikisha nchi nchi Tatu
Tanzania,Kenya,Uganda na Zanzibar imelenga kuwapatia elimu ya uelewa maafisa
hao ilikutambua thamani ya mazao ya misitu na maliasili yanayopitishwa mipakani
hususani mbao ambazo zimekuwa zikitoroshwa yakiwemo pia magogo.
Akizungumza
katika semina hiyo Mratibu wa mpango ya misitu Isaack Malugu alisema kuwa Hatua
hiyo itazisaidia nchi hizo kuokoa mamilion ya fedha yalikuwa yakipotea kutokana
na kutokuwa na uelewa wa thamani ya mazao ya misitu.
Malugu
alitaja baadhi ya mipaka ambayo imekuwa vinara wa kuvusha mazao ya misitu ikiwemo
mkaa kuwa ni pamoja na mpaka wa NamangaArusha,Hororo Tanga na Taveta
Kilimanjaro,ambapo alitolea mfano wa mpaka wa hororo kuwa kiasi cha dola million
kumi zimekuwa zikipotea kila mwaka
“Kuna Baadhi
ya miti hairuhusiwi kuvushwa bila kibali maalumu ambapo pia katika usafirishaji
kuna baadhi ya magari yamekuwa yakichanganya mbao na magogo yenye thamini kubwa
kama mloliondo mpingo na msindawe ambayo inathamani kubwa na haivunwi bila
kibali maalumu”alisisitiza Magulu
Kwa Upande
wake Ismail Aloo kutoka wakala wa misitu Tanzania alisema kuwa mafunzo hayo
yataenda sambamba na kuwajengea uelewa maofisa kutoka idara za forodha kwenye
mipaka ambapo wataweza kudhibiti mazao wa misitu kwa kutambua aina za miti
inayopita mipakani.
Alisema kuwa
hii itasaidia kudhibiti mazao ya misitu na maliasili katika mipaka yetu na
kujua thamani na kujua sheria za nchi zinazopakana nazo sheria zao zinasemaje
katika suala zima la mazao ya misitu huku serikali ikipata mapato yake halali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni