Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- MNH, Profesa Lawrence Museru amewataka wauguzi kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya Uuguzi ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma katika hospitali hiyo.
Profesa Museru ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa wauguzi Tawi la Muhimbili uliolenga kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo .
Profesa Museru amesema licha ya wauguzi hao kukabiliwa changamoto mbalimbali lakini hawanabudi kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha upendo kwa wagonjwa ili kukabiliana na ushindani na kutoa huduma bora.
“ Hii ni hospitali ya Taifa inatoa huduma za kibingwa hivyo ni lazima huduma zitolewe kwa kiwango cha juu kulingana na hadhi yake” amesema Profesa Museru.
Akisoma Risala kwa niaba ya wauguzi Katibu wa TANNA Taifa Sebastian Luziga amesema wauguzi wa MNH wanamshukuru Profesa Museru kwa jinsi anavyojitoa kuwasaidia katika mambo mbalimbali na kwamba hali hiyo inaonyesha anathamini taaluma ya uuguzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru akizungumza na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili katika mkutano uliofanyika leo hospitali hapo.
Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimsikiliza kwa makini Profesa Museru katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Wauguzi Tawi la Muhimbili .
Mkurugenzi wa Huduma ya Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Agnes Mtawa akimkabidi tuzo Profesa Museru kwa lengo la kumshukuru na kutambua mchango anaotoa kwa wauguzi wa hospitali hiyo.
Katibu wa TANNA Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tawi la TANNA MNH Sebastian Luziga akimvisha Medali Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Agnes Mtawa kama ishara ya kumshukuru kwa malezi mazuri kwa chama hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Museru akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi mara baada ya kufunga mkutano huo uliofanyika mapema leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni