Na Ahmed Mahmoud
KATIKA kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi wa wahandisi nchini,Bodi ya wahandisi (ERB) imesema imeweka mipango ya kukuza na kuimarisha weledi wa sekta ikiwemo kupambana na vitendo vya rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 10 jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Msajili wa Bodi ya wahandisi Bernad Kavishe amesema Bodi itaweka maslahi ya Umma mbele ikiwemo na kuzingatia maadili.
"Wahandisi pia lazima wadhibitiwe wawe na nidhamu na maadili mema wawe na uadilifu na kwa kifupi wahandisi tunaweka maslahi ya Umma mbele na maslah yetu binafsi nyuma na ndio maana tunachukua kiapo kuapa kuweka maslahi ya Umma mbele,
" Bodi ipo mstari wa mbele katika kupambana na rushwa manake rushwa ni adui wa uhai siyo tu adui wa haki lakini malengo mahususi ya bodi ni kuimarisha na kuhakikisha udhibiti wa kazi za wahandisi na taaluma ya wahandisi kwasababu uhandisi hauishii shuleni uhandisi ni tunahakikisha mpaka mtu ana staafu" amesema Mhandisi Kavishe
Aidha Mhandisi Kavishe ametoa wito kwa watu wenye miradi kuacha kutumia wahandisi ambao hawajasajiliwa na bodi hiyo ili kuondokana na malalamiko pale wanapoharibiwa kazi zao.
"Kinyume cha sheria kabisa kupata huduma za kihandisi nje na watu ambao hawajadhibitishwa na bodi mbalimbali za kitaaluma, ile leseni tunayokabidhi ile ndio kielelezo ambacho serikali imeipitisha kwamba huyu mtu kapata elimu sahihi hawana mashaka nae na ujuzi wake upo hai"amesema Mhandisi Kavishe.
Nae Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo barabara majengo na tayari imezalisha wahandisi zaidi ya elfu 33 na endapo miradi ikiharibiwa ERB inahusika.
"Kuna kazi kubwa inafanyika na miradi mingi ndani ya nchi yetu ambayo inategemea ushauri wa wahandisi hawa na nichukue nafasi hii kuwapongeza mpaka sasa nchi yetu imezalisha wahandisi zaidi ya elfu 33 na 26 wapo sokoni wanafanya kazi, ikumbukwe kuwa tulipokuwa tunapata uhuru mwaka 1961 tulikua na wahandisi wawili tuu leo tunazungumzia hawa walio kazini na vijana bado wapo vyuoni wanasoma wanaendelea kuzalishwa" amesema Msigwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni