TCRA YATOA LESENI 3132 KUTOKA SEPTEMBA 2021 HADI NOVEMBA 2022


 Na Ahmed Mahmoud

Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imetoa leseni 3132 katika makundi aina 6 ikiwemo leseni ndogo za ufungaji utengenezaji uagizaji usambazaji wa vifaa vya simu 2161.

Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano nchini Dkt. Jabir Bakari wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya kudhibiti anga ya mawasiliano nchi kuanzia septemba hadi novemba jijini Dodoma 

Aidha akibainisha Leseni hizo Dkt. Jabir amesema kwamba aina hizo ni pamoja na leseni za miundombinu ya mawasiliano 22, utumiaji wa miundombinu ya mtandao 10,matumizi ya huduma 107,huduma maudhui 741 television  61,mtandao 390 cable TV 65,Radio 218 sanjari na radio mtandao 7.

Kwa mujibu wa Dkt. Bakari ameendelea kuzitaja leseni hizo ni pamoja na Posta na usafirishaji wa vifurushi 91 tofauti na awali 120 huku akibainisha kwamba TCRA inasimamia shughuli za mawasiliano ya simu na inteneti kwa kuhakikisha zinatolewa kwa viwango vya kimataifa vilivyowekwa na EPOCA.

Aidha TCRA inahakikisha mifumo ya usimamizi wa mawasiliano ya simu intaneti kwa serikali kuanzisha mfumo uitwao TTMS ambao husimamia na kuratibu mawasiliano ya simu wenye uwezo wa kubaini takwimu mbalimbali zinazopita katika mitandao ya mawasiliano kwa watoa huduma.

Akabainisha kwamba TCRA imejikita kuhakikisha maudhui yanayorushwa na vituo vya utangazaji nchini yanazingatia weledi maadili wa uandishi wa habari pia hayakiuki sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya utangazaji.

Hatahivyo sekta ya mawasiliano ya simu nchini imeendelea kukua hadi kufikia septemba 2022 kulikuwa na laini za simu 58.1 milioni ambazo zinajumuisha laini zinazotumiwa na watu na mashine kwa mashine huku akieleza mikoa inayoongoza ikiwa ni Dar es Salaam laini milion 9.756 Mwanza milion 3.700 Arusha milion 3.448 Mbeya milion 3.089 na Tabora milion 3.060.

Akielezea gharama za muunganisho wa simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka 2015 zilikuwa TZS 30.58 na kwa sasa ni TZS 2.00 na kisaidia kupungua gharama za jumka za upigaji simu na kuondoa ulazima wa wateja kuwa na simu zaidi ya moja. 

Kwa muktadha huo licha ya mafanikio hayo sekta hiyo inakumbana na changamoto kadhaa ikiwemo ya uharibifu wa miundombinu ya mawasiliano, utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote maeneo ambayo hayajafikiwa mahitaji makubwa ya bendi za masafa usalama wa mtandao na uhalifu mtandao kudhibiti maudhui ya mtandao na ubora wa huduma za mawasiliano. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni