Serikali
inajipanga kwajili wataalamu wa maendeleo ya jamii 5,554 kwa kipindi
cha miaka mitano ili waweze kutoa huduma za maendeleo ya jamii
kuanzia ngazi ya Serikali kuu hadi kijiji kama ilivyokuwa kwa utawala
wa awamu ya kwanza nchini.
Ameyasema hayo katika Mahafali ya sita ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tenguru nje
kidogo ya jiji la Arusha Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Hamis Kigwangalla amesema serikali ya
awamu ya kwanza ilikuwa na idadi kubwa ya mabibi na mabwana maendeleo ya
jamii kila kata.
Aliongeza kuwa kwasasa wataalamu katika sekta ya maendeleo ya jamii wameanza
kupungua sana na kukitaka chuo kuongeza udaili wa wanafunzi ili
kuendana na azima ya serikali ya kuwa na wataalamu awa kila wilaya na
kata.
Aidha
aliitaka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuendela kutoa taaluma
yenye viwango na bora na uzingatiwe katika mchakato wote wa utoaji
mafunzo kuanzia kwenye udahili wa wanafunzi wenye sifa na vigezo ili
kujenga jamii ya wasomi wenye tija katika Taifa letu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni