DKT. KALEMANI AFANYA ZIARA KATIKA KITUO KIPYA CHA KUPOOZA UMEME CHA KURASINI NA MRADI WA KUSAMBAZA GESI MAJUMBANI


 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (katikati) akitoa maelekezo kwa watendaji  wa kampuni ya Fichtner  ya Ujerumani na Shirika la  Umeme Tanzania (TANESCO) mara baada ya kufanya ziara katika  Kituo Kipya cha Kupooza Umeme cha Kurasini kinachojengwa kupitia Mradi wa TEDAP ili kujionea maendeleo ya ujenzi wake jijini  Dar es Salaam.
 Mtaalam kutoka Kampuni ya Fichtner ya   Ujerumani, Matthias Albers (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (kushoto) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho. Katikati ni Meneja Mwandamizi (Miradi) kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gregory Chegere.
 Mafundi wakiendelea na ujenzi katika Kituo Kipya cha Kupooza Umeme cha Kurasini, kinachojengwa chini ya Mradi wa TEDAP.
 Meneja Mwandamizi (Miradi) kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gregory Chegere (kulia) akitoa maelezo  kwenye kituo cha kuendesha mitambo (control  room) katika Kituo Kipya cha Kupooza Umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mwandamizi (Miradi) kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gregory Chegere (katikati) akisisitiza jambo katika sehemu ya kupokelea laini za umeme.
 Afisa Utafiti Mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Charles Sangweni (kushoto) akimweleza Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (kushoto) kuhusu mradi wa kusambaza gesi majumbani jijini Dar es Salaam, mara alipofanya ziara kwenye makazi ya shirika hilo Mikocheni jijini Dar es Salaam ili kujionea majaribio ya mradi huo. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka  Wizara hiyo, Asteria Muhozya.
 Afisa Utafiti Mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Charles Sangweni (kushoto mbele) akimwongoza Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (katikati) kwenye ziara ndani ya makazi ya shirika hilo ili kujionea mradi wa majaribio wa kusambaza gesi majumbani.
 Afisa Utafiti Mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), (kulia) akimwonesha Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (kushoto) mita maalum kwa ajili ya kuonesha kiasi na thamani ya  gesi ( diagram meter)
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akitoa maelekezo kwa watendaji  kutoka  Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na  Wizara ya Nishati na Madini mara baada ya kumaliza ziara yake katika makazi ya shirika hilo.
Afisa Utafiti Mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni