Baadhi ya watumishi wa serikali na halmashauri wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Desemba 2, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea bahasha yenye nyaraka mbalimbali zinazoonyesha ubadhirifu unaofanyika katika halmashauri ya Wilaya ya Arusha kutoka kwa Benard Mtei wa Idara ya Afya katika halmashauri hiyo wakati alipozungumza na watumishi wa serikali na halmashauri mjini Arusha Desemba 2, 2016.
Na.Mahmoud Ahmad,Arusha.
Waziri mkuu wa Tanzani Kassimu Majaliwa ameiagiza idara ya uhamiaji kuimarisha ulinzi na ijipange kuthibiti idadi ya wahamiji nchini kwni wakizidi serikali itrashindwa kuwahudumia wahamiaji holela.
Ameyasema
haya wakati akiwazungumza na watumishi wa umma katika mkoa wa Arusha
,katika mkutano uliofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano
Aicc mkoani hapa,huku akiitaja mikoa hiyo iliyopo pembezoni ni
Kilimanjaro,Arusha,Kigoma,Tanga,na Mara.
"Tunataka kufahamu mgeni anapokuja nchini tunataka kufahamu anakuja kufanya nini ,anakaa siku ngapi,je ameingiza kitu gani nchini,Kwa mkoa wa Arusha hakikisheni mnapita kwenye nyumba za wageni kagueni vitambulisho vyao kama kweli ni watanzania kweli,na kama ni mgeni je ameingia kihalali nchini,je kitambulisho alichonacho mgeni huyo ni cha kwake kweli.?"alisisitiza waziri mkuu.
Aidha waziri mkuu amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa kuzingatia nidhamu awapo kazini,uaminifu,na uadilifu, huku wakitumia taaluma walizonazo katika sekta mliopo,kila mmoja afanye majukumu yake na kutimiza wajibu ili kuonyesha mafanikio.
"Tunataka kuona kila mtumishi wa umma anafanya kazi yenye kuonyesha mafanikio kwa wananchi ,kwa bahati mbaya sana mliyonayo watumishi ni kwamba wananchi wanaweza kufanya tathimini ,nyie kama watumishi hamtakiwi kumbagua mwananchi iwe ni kwa hali yake ya uchumi,itikadi yake ya siasa,mwananchi yeyote anayekuja ofisini kwako mpokee,msikilize,muhudumie."alisisitiza waziri mkuu.
Wakatihuohuo waziri mkuu Kassimu Majaliwa amemuagiza mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho Gambo kutoa ulinzi Bernad Mtei kwa mfanyakazi wa umma kitengo cha afya Arusha Dc kwa kufichua ufisadi unaotendeka katika wilaya hiyo Bernad Mtei.
Ameyasema hayo baada ya ndugu Bernad Mtei ambaye ni mtumishi wa umma Kitengo cha afya aliposema kuwa katika sekta hiyo ya arusha Dc kuna madudu mengi na watumishi wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu na kumuomba waziri mkuu awatatulie kero hiyo.
"Mheshimiwa waziri mkuu ili kuhakikisha ninayoyazungumza ni kweli kwanza naomba unilinde maana nikitoka hapa naweza hata kufanyiwa jambo baya maishani mwangu,kwani tayari nimekuwa nikipokea jumbe mbalimbali za kunitishia kupitia simu yangu ya kiganjani,naomba unilinde mheshimiwa,pia naomba nikuabidhi kabrasha hili lenye nyaraka za uharibifu unaotendeka katika Arusha Dc.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni