VIONGOZI KUTOKA VYAMA VYA SIASA WAKIFUATILIA WARSHA HIYO |
sehemu ya washiriki wakifuatilia warsha hiyo |
WAHARIRI WA REDIO ZA JIJINI ARUSHA Baraka Sunga na Joseph Laizer AIDEA FM NA SUNRISE WAKIWA NA MWANDISHI WA CLOUDS TV Beatrise gerald |
Makundi yakichangia maoni yao katika warsha hiyo |
Wagombea wanawake waliogombea kwenye uchaguzi mkuu uliopita wilayani Meru wakiteta jambo wakati wa warsha hiyo |
Kundi la waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali walioshiriki warsha hiyo wakijadiliana mada kwenye warsha hiyo ya siku mmoja |
WAGOMBEA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAKIFUTILIA WARSHA HIYO ILIYOANDALIWA NA TAMWA NA UN WOMEN KWA WAGOMBEA WAANDISHI WA HABARI VIJANA NA MAKUNDI MAALUMU |
Washiriki wakifuatilia jambo wakti semina ikiendelea |
Na Mahmoud
Ahmad Arusha
Wadau wa
maendeleo,viongozi wa siasa na vyombo vya habari wanalojukumu la kuhakikisha
wanahamasisha wanawake, makundi maalum na vijana kuomba nafasi za uongozi kwa
wingi ilikuweza kuwa na usawa wa kijinsia kwenye masuala mbalimbali ya
kujiletea Mandeleo,
Hayo
yamebainishwa kwenye warsha ya siku moja iliyowashirikisha wagombea
wanawake,makundi maalum na vijana,wanahabari, pamoja na viongozi wa vyama vya
siasa iliyoandaliwa kwa pamoja na TAMWA na UN WOMEN na kufanyika wilayani
Arumeru mkoani hapa.
Akizungumza
wakati akitoa mada mratibu wa semina hiyo Rashida Shariff alisema kuwa warsha
hiyo ni kushirikiana matokeo ya ripoti ya uchambuzi na kujadili changamoto
walizopata wagombea wanawake,makundi maalumu na vijana katika kipindi cha uchaguzi kwa vyombo vya habari hapa nchini kutoripoti
ipasavyo habari zao kutokana na vyombo hivyo kuwa ni vya kibiashara zaidi.
Alisema kuwa
malengo ya warsha hiyo ni kujadili changamoto za uchaguzi mkuu na nini
kifanyike,ambapo wanatambua vyombo vya habari
ni chanzo mojawapo katika kuwatoa wananchi katika giza na kuwapeleka
katika mwanga ili kusaidia na kuibua changamoto ya kuweza kufikisha taifa
katika usawa wa kumfanya mwanamke,makundi maalumu na vijana kuwa nao wanauwezo
sawa na wengine ambapo wanasiasa
wanawake,makundi maalumu na vijana kama watapewa kipaumbele cha kupata nafasi
ya habari zao kuripotiwa na vyombo hivyo kila mara.
“Warsha hii
ni kufuatilia jinsi vyombo vya habari vilivyoripoti taarifa za wanawake na
vijana katika kugombea kwenye uchaguzi mkuu uliopita na kupata uchambuzi wa
dhana ya kijinsia katika vyombo vya habari juu ya usawa wa kijinsia katika
huduma za jamii na uongozi”alisema Shariff
Kwa upande
wake Katibu wa chama cha wananchi (CUF)mkoani hapa Zuberi Mwinyi alisema kuwa
lazima kuwe na mabadiliko kwa wanahabari kupewa semina za mara kwa mara
ilikusaidia wanawake,makundi maalumu na vijana kwa sababu tasnia ya habari ndio
nyenzo ya kumtoa mtu kutoka eneo moja kwenda jingine.
Alisema kuwa
tofauti na hapo watanzania watajiona hakuna kinachoendelea kwa kuwa hakuna
tathmini ya mabadiliko katika sekta ya kuwasaidia wanawake,makundi maalum na
vijana iliweze kufikia malengo ya kuwa na usawa wa kijinsia katika jamii
wanaoishi.
Nae Mjumbe
wa halmashauri kuu ya Uvccm mkoani hapa Saitoti Zelothe alisema kuwa ifike
mahali wanawake,makundi maalum na vijana wakasaidiwa kukuwa kiuchumi na kuweza
kwenda sambamba na wagombea wengine kwani suala la gharama za kifedha katika
uchaguzi halikwepiki na limekuwa mwiba kwa wagombea wa kundi hilo kukosa mwamko
wa kugombea.
Mwisho…………………………………………………………….
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni