Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Arushaa ofisini kwake
juzi kutoka vyombo mbalimba vya habari kuhusu sakata la kukamatwa
kwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha ITV Halfani
Liundi ambapo amehaidi kulishughulikia huku akiwataka waandishi
kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mwandishi wa kituo
cha ITV Halfani Liundi aliyekamatwa hivi karibuni na jeshi la polisi,
ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa anatambua umuhimu wa
vyombo vya habari na hivyo mwandishi ana uhuru wa kwenda popote kupata
taarifa yeyote kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa habari
Mwandishi wa habari wa kituo cha
channel Ten Aristrides Dotto akichangia katika mkutano huo wa
waandishi wa habari na mkuu wa Mkoa juzi ofisinii kwake jijini Arusha
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifatilia mkutano huo
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi
Mosses Mashalla akichangia katika mkutano huo wa mkuu wa Mkoa na
waandishi wa habari mkoa wa Arusha. (Picha zote na Mahmoud Ahmad arusha)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni