Mhariri
Mtendaji wa gazeti la Mtanzania, Absalom Kibanda akimfariji mjane wa
marehemu Mpoki Bukuku, Lilian nyumbani kwa marehemu, Tabata Bwawani, Dar
es Salaam. Bukuku alifariki juzi baada ya kugongwa na gari Barabara ya
Bagamoyo karibu na Kituo cha ITV, Mwenge. PICHA NA RICHARD
MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kibanda akimfariji mama mzazi wa marehemu Mpoki Bukuku
Kiongozi
wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe (kulia) akizungumza jambo na Shemeji wa
marehemu Mpoki Bukuku, Edwin Mjwahuzi alipokwenda kuwafariji wafiwa
nyumbani kwa marehemu, Tabata Bwawani.
Zitto Kabwe (kulia) akizungumza na kaka wa Marehemu Mpoki, Gwamaka Bukuku wakati wa msiba huo
Waandishi wa habari wakiwa kwenye msiba wa marehemu Mpoki Bukuku ambaye
alikuwa Mpigapicha mwandamizi wa magazeti ya Kampuni ya The Guardian
Wanahabari wakijadiliana mambo wakati wa msiba huo
Mmiliki
wa Blogu hii, Kamanda Richard Mwaikenda, ambaye pia ni Mpigapicha Mkuu
wa gazeti la Jambo Leo, Kamanda Richard Mwaikenda (kulia) akiwa na
wanahabari wenzie kwenye msiba huo.Kutoka kushoto ni Mpigapicha wa
Waziri Mkuu, Hilary Bujiku, Mmiliki wa Blog ya K-VIS, Khalfan Said,
Mmiliki wa Blog ya Michuzi, ambaye pia ni Mpiga Picha na Mwandishi wa
Habari Msaidizi wa Rais, Muhidini Issa Michuzi, Mpigapicha Mkuu wa
Gazeti la Mwananchi, ambaye ni shemeji wa marehemu Mpoki, Edwin Mjwahuzi
na Francis Chirwa ambaye ni mmoja wa viongozi wa Bodi ya Wahariri wa
Gazeti la Raia Mwema.
Waombolezaji wakiwa kwenye msiba
Jirani rafiki wa karibu wa marehemu, Mpoki, maarufu kwa jina la Mijisu akilia wakati wa msiba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni