Kampuni
ya Magazeti ya Serikali (TSN) Wachapaji wa magazeti ya Daily News,
Sunday News, Habarileo, Habarileo Jumapili na Spotileo imeadhimisha
miaka 10 tangu kuanza kwa gazeti la Habarileo mnamo Desemba 21, 2006 kwa
kukata keki huku Uongozi wa Kampuni hiyo ukitangaza shamra shamra za
mwezi mmoja wa kusherehekea kuzaliwa kwa gazeti hilo.
Aidha
ili kushirikiana na wadau wengine, Kampuni imetangaza punguzo la
asilimia 30 kwa mteja atakeatangaza tangazo lake ndani ya siku 30 za
shamrashamra katika gazeti la Habarileo.
Miongoni
mwa wageni maalum waliohudhuria sherehe hizo ni Mhariri Mtendaji wa
zamani wa TSN, Isack Mruma (wapili kulia) ambaye kwa sasa ni Ofisa wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambaye alishiriki kukata keki
pamoja na Mhariri Mtendaji wa sasa Dk Jim Yonaz (wapili kushoto) na
Naibu Mharidi Mtendaji, Tuma Abdallah. Kushoto akishuhudia ni Meneja
Mauzo na Masoko, Januarius Maganga.
Naibu Mharidi Mtendaji, Tuma Abdallah akimlisha keki Kaimu Mhariri wa Gazeti la Habarileo, Nicodemus Ikonko.
Shangwe za miaka 10 ya Habarileo.
ME wa zamani wa TSN Isack Mruma akilishwa keki na ME wa TSN Dk Jim
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni