MWILI WA BALOZI WA URUSI ALIYEUWAWA ANKARA WAWASILI MOSCOW



Mke wa Balozi Andrei Karlov amebubujikwa na machozi wakati mwili wa mumewe ukiwasili nchini Urusi na kupokelewa wanajeshi baada ya kuuwawa jumatatu kwa kupigwa risasi Jijini Ankara nchi Uturuki.

Maria, mama wa Balozi huyo alipata wakati mgumu kuzuia machungu yake wakati jeneza lililokuwa na mwili wa mwanae lililofunikwa na bendera ya Urusi likibebwa na wanajeshi katika uwanja wa Kimataifa wa Vnukovo Jijini Moscow.
                          Wanajeshi wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa balozi Andrei Karlov 
Mke wa balozi, Marina mwenye nguo nyeusi akiwa na mama mkwe wake Maria wakilia kwa uchungu huku wakishika jeneza

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni