MAAFISA USALAMA UJERUMANI LAWAMANI KWA UZEMBE SHAMBULIZI LA BERLIN


Makosa ya mfululizo ya kiusalama yamepelekea kumuacha mhamiaji hatari kutoka Tunisia kuwa huru na kufanya shambulizi la kutumia lori Jijini Berlin katika soko la Krismasi.

Kikosi cha Usalama cha Ujerumani kinawakati mgumu wa kujibu maswali baada ya kubainika mtuhumiwa huyo Anis Amris alikuwa na rekodi za uhalifu na alipaswa kurejeshwa kwao miezi kadhaa iliyopita.

Amris, 24, ambaye sasa anasakwa na limetangazwa donge nono la Euro 100,000 kwa atakayefanikisha kukamatwa kwake, alikuwa chini ya uangalizi kwa miezi kadhaa tangu 2015.
                  Lori lililotumika kufanya mauaji ya watu 12 na kujeruhi wengine Jijini Berlin
       Baadhi ya wahamiaji wakiweka maua katika eneo la tukio kuomboleza watu waliouwawa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni