Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (kulia),
akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi
(kushoto) wakati akielezea mafanikio na changamoto zinazokikabili chuo
hicho. Kushoto kwa Mkuu wa Chuo ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali
Bw. Mohamed Mtonga, Msaidizi wa Mkuu wa Chuo Dkt. Samwel Werema,
Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi– Ukaguzi Mamlaka za Mitaa Bw. Mwanyika
Musa na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Kiufundi Bw. Amin Mcharo
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (kulia),
akijibu hoja zilizotolewa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt.
Faraji Kasidi (kushoto) alipofika Ofisi Kuu ya Chuo hicho kabla ya
kufungua mafunzo ya siku nne ya wakaguzi kutoka mikoa ya Kanda ya
Kaskazini.
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi aliyesimama akitoa
utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo
kwa wakaguzi wa Ndani kutoka Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa.
Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi.
Doroth Mwanyika, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Mohamed Mtonga, Mkuu
wa Kitengo cha Ukaguzi wa Kiufundi Bw. Amin Mcharo na kulia kwa Kaimu
Mkuu wa Chuo ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali – Ukaguzi
mamlaka za mitaa Bw. Mwanyika Musa.
Wakaguzi
wa Ndani kutoka Serikali za Mtaa na Sekretarieti za Mikoa wakiwa kwenye
mafunzo ya ukaguzi, Mgeni Rasmi katika mafunzo hayo ni Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika. Mafunzo haya
yanafanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, mkoani Arusha.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika
(aliyesimama) akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa ndani
ambapo alisema mpaka sasa wakaguzi wa ndani 308 wamepata mafunzo hayo
na wakaguzi 32 wameshafanya mafunzo hayo kwa vitendo.
Wakaguzi
wa Ndani kutoka Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa katika picha
ya pamoja. Waliokaa ni Mgeni Rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
na Mipango Bi. Doroth Mwanyika kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha
Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa
Kiufundi Bw. Amin Mcharo na kushoto kwake ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa
Serikali Mohamed Mtonga na Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali –
Ukaguzi mamlaka za mitaa Bw. Mwanyika Musa.
Mgeni
Rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth
Mwanyika (katikati) wakibadilishana mawazo na Kaimu Mkuu wa Chuo cha
Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi (Kushoto) na kulia ni Mkaguzi wa
Ndani Mkuu wa Serikali Mohamed Mtonga.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika akimsikiliza
Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali – Ukaguzi mamlaka za mitaa
Bw. Mwanyika Musa ambapo alisema mafunzo hayo ni muhimu kwani yamelenga
kuimarisha ukaguzi wa miradi mikubwa ili ujenzi wake ulingane na thamani
ya fedha iliyotumika.
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi akumfafanulia jambo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika.
Mahmoud Ahmad, Arusha
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika, amewataka wakaguzi wa ndani nchini kuhakikisha kuwa miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara na majengo yanajengwa kwa ubora unaolingana na thamani ya rasilimali fedha iliyotumika.
Bi. Mwanyika ametoa rai hiyo Jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya wakaguzi wa ndani kutoka Halmashauri za wilaya na Sekretarieti za mikoa iliyoko Kanda ya Kaskazini, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara
Amesema kuwa wabunge na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakilalamikia miradi mingi mikubwa ikijengwa chini ya kiwango na kuisababishia serikali hasara kubwa kutokana na usimamizi mbovu unaofanywa na mamlaka na idara za serikali wakiwemo wakaguzi wa ndani.
“Nina Imani kuwa mafunzo mnayoyapata ya namna ya kukagua ubora wa miradi mikubwa inayotumia fedha nyingi za serikali yatasaidia kuokoa fedha na kuifanya miradi inayojengwa idumu muda mrefu” aliongeza Bi. Mwanyika.
Kwa upande wake Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali Bw. Mohammed Mtonga, amesema kuwa kuanzishwa kwa mafunzo hayo yanayofadhiliwa kupitia mradi wa kuboresha Mifumo ya Fedha (PFMRP), yanatokana na mahitaji makubwa ya ujuzi wa namna ya wakaguzi wa ndani wanavyoweza kutambua ubora wa miradi mikubwa ya ujenzi inayotekelezwa hapa nchini kama inakidhi viwango.
“Wakaguzi hawa si wataalamu wa masuala ya ukandarasi lakini uwezo wanaojengewa ni pamoja na kupelekwa kwenye miradi mikubwa ya uejnzi ikiwemo barabaraba ambapo wataelekezwa namna ya kutambua miradi ambayo haikidhi viwango na kutoa ushauri kwa watoa maamuzi ili kuokoa fedha ya serikali isipotee” aliongeza Mtonga.
Wakaguzi wa ndani 302 kutoka Halmashauri na Sekretarieti za Mikoa nchini wamepatiwa mafunzo hayo ambapo pamoja na mafunzo ya nadharia, wakaguzi hao wa ndani wamefundishwa kivitendo namna ya kutambua miradi iliyojengwa chini ya viwango

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni