| |||||||
|
Na.Mahmoud Ahmad
Arusha
Mwanamuziki wa kizazi kipya Ben Pol ambapo kwa watu wengi
wanamtambua kwa wimbo wake wa moyo mashine amezikonga nyoyo za wakazi
wa Arusha walipokuwa wakisheherekea sikukuu ya Christimas katika
ukumbi wa Mjengoni Club uliopo Olasiti Jijini Arusha.
Awali kuliibuka uvumi kuwa msaniii huyo hatatokea katika shoo hiyo katika usiku huo wa kusheherekea sikukuu christimas jambo ambalo lilizua sintofahamu kwa baadhi ya watu walioingia ukumbini hapo kwaajili ya kumuona Ben Pol. Blog hii ilipata muda wa kuzungumza na mkurugenzi wa Mjengoni Klub John Mdeme pamoja na Kiongozi wa Bendi ya Mjengoni Classic Robert Mukongya ili kutaka kufahamu kuhusiana na uvumi huo ndipo walipojibu kwa kusema kuwa hayo ni maneno tu ya upotoshaji . "Jamani sijui nani kazileta taarifa hizi kwani Ben tulikuwa nae mchana kwenye shoo ya watoto ,sasa haya yametoka wapi binadamu bwana!mimi nakuaminisha Ben yupo na watu wote waliopo hapa watafurahi na kuburudika mioyoni mwao wala wasitie shaka"alisisitiza John. Aidha mkurugenzi huyo alisema kuwa waliamua kuwaandalia kitu kizuri wakazi wa Arusha kwa bendi ya Mjengoni Classic pamoja na Ben Pol kuwepo kuwapa raha wakazi wa Arusha na wageni mbalimbali kutoka nje ya Arusha na nchi mbalimbali waliokuja kusheherekea sikukuu wapate ladha tofauti na nzuri. | |||||
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni